Na Gideon
Mwakanosya-Songea
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limewatia mbaroni watu watatu
ambao walikamatwa wakiwa na bunda kumi
za karatasi zenye sura ya Dora mia moja ambapo kila bunda moja lina karatasi 86
zenye thamani ya shilingi milioni 86 za kitanzania .
Watuhumiwa waliokamatwa
wametajwa kuwa ni Bonifasi Simwanza(41) ambaye ni raia wa nchi ya
Zambia, Adam Msongole(26)mkazi wa mji mdogo wa Tunduma uliopo wilayani Momba
mkoa wa Mbeya uliopo mpakani mwa Tanzania na Zambia na Hatmani Steven(29) Mkazi
wa eneo la Makumbusho kijitonyama jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Nipashe jana ofisini kwake kamanda wa polisi
wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea April 19
mwaka huu majira ya saa 7 mchana huko katika eneo la Mtaa wa Oil Com Petrol
station mjini kati manispaa ya songea.
Alieleza zaidi kuwa siku hiyo ya tukio Afisa upelelezi wa
makosa ya jinai wa mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi akiwa ameongozana na askari
walifanikiwa kuwakamata watu watatu wakiwa na karatasi za kutengenezea noti
bandi.
Alifafanua zaidi kuwa askari hao walikamata bunda kumi za
karatasi zenye sura sawa na dola mia moja ambapo kila bunda moja lina karatasi 86 na baadhi ya
vitu vingine ambavyo alivitaja ni mkasi mmoja, Gloves mbili na pamoja na
karatasi nyeusi ambazo zinadaiwa kuwa ni malighafi za kutengenezea dola.
Kamanda Msikhela alieleza kuwa jeshi la polisi mkoani humo
linaendelea kufanya uchunguzi wa kina na baada ya kukamilisha uchunguzi huo
watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
MWISHO.
Chapisha Maoni