Press ? for keyboard shortcut
HALI ya sintofahamu imejitokeza katika miradi ya maji
inayotekelezwa katika halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma baada ya
Naibu Waziri wa Maji Amos Makala kubaini ubadhilifu mkubwa wa fedha za miradi
ya maji kujengwa chini ya viwango na mingine kutokamilika licha ya fedha hizo
kulipwa zote wakandarasi.
Kufuatia hali hiyo amesema kuwa atakaporudi Wizarani
atamuandikia katibu mkuu wizara ya maji atume kikosi kazi ambacho kitaenda
kufanya uchunguzi wilayani Namtumbo ndani ya wiki mbili na amemuomba mkuu wa Mkoa
pamoja na mkuu wa Wilaya kuwapa watu wa TAKUKURU ili iwe timu iliyokamilika
bila kumuonea mtu.
Alisema
kuwa serikali imekuwa itumia fedha nyingi kwa aajiri ya kutekeleza
miradi ya maji vijijini na mijini lakini hawa watu wanafanya dili na
kama Wizara itahakikisha mtandao huo unavunjwa ili kukomesha kabisa
vitendo vya watu kuandika miradi kwa gharama kubwa badala yake miradi
inayotekelezwa inakuwa chini ya viwango na haikidhi mahitaji ya
wananchi.
Hayo yamebainika jana wakati akipewa taarifa ya Wilaya hiyo
juu ya uteke;lezaji wa ilani wa CCM katika miradi ya maji ambapo mkuu wa Wilaya
hiyo Agnes Hokololo alisema kuwa wanatatizo na mhuandisi mshauri kwani ndiye
amekuwa tatizo kwenye utekelezaji wa miradi hiyo jambo ambalo limewatia hasira
wananchi wa kijiji cha Milonji.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa halmashauri ilitakiwa
kujenga mradi wa viosima viwili virefu vyenye mita 150 lakini hadi sasa
kimechimbwa kimoja ambacho nacho kinaurefu wa mita 71 na kwamba kutokana na
kupunguza kina cha urefu wa kisima kimesababisha kupunguza mita za ujazo 2500
za maji kwa saa badala ya awali ambayo ingetoa mita za ujazo 9000.
Alieleza zaidi kuwa kutokana na hali hiyo wananchi wa kijiji
cha Milonji wamekataa mradi huo jambo ambalo limesababisha viongozi wanaoenda
kijijini hapo kuimiza shughuli za maendeleo zikwame kwa kuwekewa magogo njiani
hadi hapo mkandarasi atakaporekebisha ujenzi wa miradi hiyo kama ilivyatakiwa
kwenye zabuni.
Pia alisema kuwa kuna tatizo jingine kwenye miradi hiyo
ambapo mkandarasi pamoja na mhandisi mshauri wamebadilisha manunuzi ya kununua
umeme jua badala yake wamenunua jenereta dogo la KVA 31 badala ya KVA51 ambalo
lingeweza kupampu maji kwenye kina kirefu lakini kwa sasa jenereta lililofungwa
halikidhi mahitaji ya wananchi wa kijiji cha Milonji.
‘’Mh naibu Waziri miradi hiyo ambayo hadi kukamilika
imegharimu kiasi cha sh bilioni 724,565,490 inaonekana inachangamoto katika
utekelezaji ,ikiwa ni pamoja na kasi ndogo ya wakandarasi kutekeleza na
kukamilisha miradi hiyo kimsingi inaonekana mhandisi msahauri katika miradi
yote hii haoni umuhimu wa kukamilisha miradi kwa wakati na hiyo inatokana na
kushindwa kutoa ushauri unaofaa kwa wakati jambo ambalo linasababisha
malalamiko mengi kwa wananchi na kukosa imani kwa serikali yao.”alisema Kuu wa
Wilaya Hokololo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa maji Makala alionesha
kusikitishwa na kusuasua kwa miradi hiyo na ubadhirifu wa fedha unaofanywa na
mhandisi mshauri,mkandarasi pamoja na wakuu wa idara ya sekta ya maji kwani
zabuni inaonesha kuwa kampuni ya mkongo constraction pamoja na Berasi Invesnent
ndio waliotakiwa kutekeleza miradi hiyo kwa makubaliano yaliyopo kwenye zabuni.
“Katika Wilaya ambazo nimepita Wilaya yenye halufu ya
ufisadi mkubwa kwenye miradi ni Namtumbo na mimi kama naibu waziri wa maji
sitakubali kusikia naitwa waziri mzigo huku
nitakiwa kuwajibishwa sitakubali kuwajibishwa hivyo ninaanza na wachini
yangu na hapa nawahakikishia nitatuma kikosi kazi ambacho kitakuja kufanya
uchunguzi kwenye miradi hiyo ndani ya wiki mbili wakiwa na jopo la watu wa TAKUKURU.”alisema
Makala.
Alisema kuwa kikosi kazi hicho kitakapo kuja namtumbo
ameitaka ngazi ya Mkoa na Wilaya kutoa ushirikiano ili waweze kufanya kazi kwa
haraka na hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Chapisha Maoni