0



NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuwadhamini makada waliotangaza nia ya kuutaka urais wasio na chembe chembe za rushwa wala ufisadi ili kuweza kuwapata viongozi wazuri wanaotokana na chama hicho

Wito huo umetolewa jana kwenye ukumbi wa ccm mkoa wa Ruvuma na Balozi Dkt Agustino Mahiga wakati alipokuwa akiongea na wanachama wa ccm waliofika kumdhamini katika safari yake ya kinyanganyiro cha urais

Dkt Mahiga alisema kuwa akifanikiwa kupata Urais Serikali yake itapambana kikamifu na maradhi  yariyokithiri ya rushwa na ufisadi uliosababisha umasikini na baadhi ya wahisani kuthitisha misaada ambayo ilikuwa ni ya maendeleo kwa watanzania

Alisema kuwa wahisani wamekuwa wakimlalamikia sana kwa kuja Tanzania kuwekeza katika miradi mbalimbali lakini wamekuwa wakikutana na changamoto nyingi ikiwemo rushwa na ufisadi kutoka kwa baadhi ya viongozi wa idara na taasisi za serikali hali ambayo imewafanya wahisani hao kusitisha malengo yao

Alisema anashangaa sana kuwa baadhi ya walioharibu heshima ya nchini na mwelekeo wa kiuchumi nao wamechukua fomu ya kugombea nafasi ya uteuzi wa urais na kuwafanya watanzania wachanganyikiwe

Alisema kuwa mara baada ya kupata nafasi ya urais hatahakikisha anawashughulikia kikamilifu  wala rushwa na wabadhilifu ili heshima ya nchi irudi kama alivyopiacha muasisi wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere

“kuna mambo mengi sana ambayo nitayafanya mara baada ya kuteuliwa na vikao vyangu vya chama  kwa kufuata ilani ya ccm ili kuwaletea wananchi maendeleo ila kwa leo nawashukuru kwa kuniambini na kwa kuja kwenu kunidhamini”alisema Dkt Mahiga

Chapisha Maoni

 
Top