NA STEPHANO
MANGO,SONGEA
CHAMA cha
Mapinduzi (CCM) kimetakiwa kumsimamisha mgombea bora mwenye kukivusha chama salama kwenye uchaguzi
mkuu ujao na sio kuangalia uzoefu wa mgombea katika siasa za Tanzania kwani
Rais wa Kwanza Mwalimu Nyerere alikuwa Mwalimu wa Sekondari na hakuwa na uzoefu
wa Urais
Wito huo
umetolewa jana kwenye ukumbi wa ccm mkoa wa Ruvuma na Naibu waziri wa fedha
Mwigulu Nchemba alipokuwa anawahutubia wanachama waliojitokeza kumdhamini ambao
walikuwa 45 katika safari yake ya kuwania nafasi ya uteuzi wa kugombea Urais ndani
ya chama chake
Nchemba
alisema kuwa muda umefika wa Taifa hili kuongozwa na kijana ambaye ni naibu Waziri
wa Wizara ya Fedha kwani changamoto nyingi anazijua na ameishi nazo na wala sio
muhimu kuongozwa na watu wanaojiita kuwa ni wazoefu wa Urais
Alisema kuwa
kuna baadhi ya wagombea wanajiita kuwa wao ni wazoefu kwenye nafasi ya urais ni
waongo kwani wanawadanganya wanachama mchana kweupe kwani wenye uzoefu wa
nafasi hiyo ya urais ni Rais Mstaafu Alli Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa,
Jakaya Kikwete na Marehemu Mwalimu Julius Nyerere
Aliwapongeza
viongozi wote wa Serikali kwa awamu nne zilizopita ambao waliweza kutengeza
misingi imara ya uchumi, miundombinu, elimu na utawala bora na kuwafanya watanzania
waendelee kuishi kwa amani na huru
Alisema kuwa
akifanikiwa kupata dhamana ya kupeperusha bendera ya Taifa atahakikisha
anakomesha tabia mbaya iliyokithiri ya kufanya kazi kwa mazoea na kuwafanya
wananchi wasipate huduma bora na kwa wakati
Alieleza
kuwa atafanya mambo makubwa ya kuboresha uzalishaji wa mazao mbalimbali ya
wakulima kwa kila ukanda ili kuwafanya wananchi waendane na uchumi imara na sio
kuwafanya wawe na uchumi dhaifu
MWISHO
Chapisha Maoni