CHUO CHA VETA SONGEA CHAPATIWA MSAADA WA GARI YA
MAFUNZO TOKA USAID. TAREHE 02/06/2015
Mwanzoni
mwa mwezi Aprili mwaka 2014 Chuo cha VETA Songea chini ya usimamizi wa Ofisi ya VETA Kanda ya nyanda za juu kilikubali ombi kutoka shirika la IYF
la kutoa mafunzo kwa vijana
wanaoishi katika mazingira magumu ili
waweze kupata elimu ya mafunzo ya ufundi stadi
katika kozi fupi, katika fani mbalimbali. Mafunzo hayo
yamekuwa yakiratibiwa kupitia mradi wa Tanzania
Youth Scholars (TYS) unaotekelezwa
na shirika na
Internation Youth Foundation (IYF) chini
ya Ufadhili wa Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kuzuia maambukizi ya Ukimwi kwa
kifupi- PEPFAR kupitia shirika la misaada la marekani yaani
USAID.
Lengo
la utoaji wa mafunzo hayo kwa watoto wanaotoka katika mazingira magumu
(wasiokuwa na uwezo) ni kuwasaidia kuongeza kipato kwa
kujiajiri au kuajiliwa baada ya kuhitimu mafunzo yao na hivyo
kupunguza uwezekano wa kupata mambukizi ya ukimwi kwa kutokuwa wategemezi.
Hadi
sasa mafunzo hayo yametolewa katika awamu mbili tofafuti ambapo awamu ya kwanza
ilianza tarehe 23/06/2014– 07/11/2014,
awamu ya pili inaendelea ambayo ilianza tarehe13/04/2015. Watoto wanaopata mafunzo hayo ni wale wanaotoka Songea mjini na vijiji vinavyozunguka
Manispaa.
Akipokea
msaada huo mkuu wa Chuo amebainisha kwamba wanafunzi hao wameweza kupata faida
mbalimbali ikiwa ni pamoja na:-
1
.
Kupata mafunzo
yatakayo wasaidia kujiajiri.
2.
Kupata mafunzo ya
ujasiriamali ili waweze kwenda sambamba na mahitaji ya soko.
3.
Kuunda vikundi vya
ujasilia mali.
4.
Kupatiwa vifaa vya
kufanyia shughuli za ujasiliamali kulingana na fani walizosoma.
Akikabidhi
msaada wa magarimwakilishi
kutoka USAID bi Laura Kikuli alisema
USAIDwametoa msaada huo ili uweze kutumika katika kufundishia vijana watakao chukua mafunzo ya kuendesha na kutengeneza magari.
Makabidhiano hayo
yalifanyika Ofisi ya VETA Kanda ya Dar-es-salaam. Wakati akikabidhi magari
hayo alisema kwamba vijana wengi wa
nchi zinazoendelea (Tanzania)wamekuwa wakikaa pasipo kuwa na kazi maalumu
zakufanya.
Kwa
kutambua hilo shirika la misaada la Marekani (USAID) kupitia International
Youth Foundation pamoja na kutoa misaada mingine kwa watoto wanaotoka katika
mazingira magumu wameona ni vyema kuviongezea uwezo vyuo vya VETA kwa kuvipatia
msaada wa magari na vifaa vingine vitavyosaidia vijana kujifunza.
Kwa mwaka
jana , walitoa magari mawili na AC units 6 zilitotumika katika chuo cha VETA dar es salaam vyote
vikiwa na lengo la kuimarisha ufundishaji kwa vitendo na mwaka huu wametoa gari moja moja katika vyuo viwili vya VETA Songea na VETA Chang’ombe.
Nae
mkurugenzi wa mradi kutoka IYF, bi Sarah Shebele, alisisitiza kwa kusema kwamba
lengo lakutoa msaada wa magarihayo ni pamoja
na:-
·
Kuwawezesha VETA
ambao ni wadau wakubwa wa utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi kupata magari ambayo
yatawawezesha kutoa mafunzo bora ya vitendo kwa vijana
wengi zaidi na hatimaye kuweza kujiajiri au kuajiriwa.
Akitoa shukurani kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu
wa VETA, Mkurugenzi wa VETAKanda ya Dar es salaam Ndugu Bhuko alisema,magari hayo yatatumika kwa lengo lililokusudiwa
pamoja na kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi.
Sambamba
na shukurani hizo aliomba misaada hiyo iendelee kutolewa katika vyuo vingine vya
VETA.
Chapisha Maoni