0
MSHINDI WA KURA ZA MAONI CHADEMA  JIMBO LA SONGEA MJINI JOSEPH FUIME
NA STEPHANO MANGO,SONGEA


WAKATI watia nia wa nafasi ya udiwani na ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi katika jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma wakiendelea na kampeni za ndani ya chama hicho chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wilayani Songea kimekamilisha mchakato wa uchaguzi wa kura za maoni za kumpata mgombea wa nafasi ya ubunge kwa tiketi ya chama hicho.


Mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo kikuu huria tawi la Songea ambao ulihudhuriwa na jumla ya wajumbe 214 wakiwemo wagombea sita waliojitokeza kuwania nafasi hiyo kwenye kinyang’anyiro hicho.


Waliojitokeza kutia nia ya kuwania nafasi hiyo ni Stella Mapunda ambaye ni mfanyakazi wa benki ya biashara ya India tawi la Tanzania lililoko Dar Es Salaam, Neema Komba ambaye ni mwalimu mstaafu na pia mwanaharakati wa mashirika yasiyo ya kiserikali jijini Dar Es Salaam,Fredrick Fussi ambaye ni mshauri na mkaguzi binafsi wa mahesabu jijini Dar Es Salaam,Dkt.Walter Ngonyani ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa akina mama ambaye kwa sasa anajishughulisha na biashara binafsi za maduka ya dawa muhimu na zahanati zilizopo jijini Dar Es Salaam na wengine ni pamoja na Mussa Ndomba ambaye ni mfamasia katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma na diwani mstaafu wa kata ya mjini Manispaa kwa tiketi ya chama hicho Joseph Fuime.


Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa uchaguzi mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Songea John Mwankina amesema wagombea ubunge kupitia chama cha demokrasia na maendeleo  walijitokeza wanachama sita ambapo katika uchaguzi huo Joseph Fuime ambaye alikuwa diwani wa kata ya Songea mjini aliibuka kuwa mshindi kwa kupata kura 139 kati ya kura 214 zilizopigwa.


Amesema kuwa kura mbili kati ya hizo ziliharibika na alitaja idadi ya kura za kila mgombea kuwa ni Fredrick Fussi(7),Stella (5),Neema(5),Dkt Ngonyani(22),Ndomba(46) huku Fuime akipata kura 139 na wagombea wengine ambao kura zao hazikutosha waliliridhika na matokeo hayo na mbele ya wajumbe wa mutano mkuu huo kuwa watahakikisha kuwa mgombea  mwenzao Fuime anapata ushindi katika ucgaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu na kwenye kikao cha kwanza bunge lijalo watamsindikiza na kushuhudia kuapishwa kwake kuwa mbunge wa jimbo la Songea mjiini kupitia chama hicho.


Mwisho.

Chapisha Maoni

 
Top