KADA WA CHADEMA MUSSA Mussa Abdallah Ndomba
MUSSA NDOMBA KADA WA CHADEMA ANAYEJITOSA UBUNGE JIMBO LA SONGEA MJINI 2015
STEPHANO MANGO,SONGEA
JIMBO la Songea Mjini
lipo katika wilaya ya Songea mkoa wa Ruvuma linajumla ya kata 21 za
kiutawala na kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni miongoni mwa
Halmashauri 6 zinazounda Mkoa wa Ruvuma na kwamba Halmashauri hiyo ipo kati ya
nyuzi 9010 hadi 11035 kusini mwa ikweta na nyuzi 35010 hadi nyuzi 35045
mashariki
Kwa upande wa kaskazini halmashauri hiyo inapakana na
halmashauri ya wilaya ya Songea na Namtumbo na upande wa kusini, mashariki na
magharibi halmashauri ya manispaa inapakana na halmashauri ya wilaya ya Songea
Jimbo hilo lina eneo lenye ukubwa wa jumla ya kilometa za
mraba 616.36 ambapo wastani wa asilimia 90 ya eneo hili linafaa kwa shughuli za
kilimo na ufugaji ambalo ni sawa na kilometa za mraba 557.36 na kwamba eneo
lenye kilometa za mraba 12.9 linafaa kwa makazi na shughuli za uzalishaji mali
viwandani na kilometa za mraba 46.1 ni milima, mabonde, misitu na mito
Kutokana na matokeo ya sense ya mwaka 2012 jimbo la Songea
Mjini ilikuwa na watu 203,309 kati ya hao wanaume walikuwa ni 96,097 na
wanawake walikuwa ni 107,212 na kwamba ongezeko la watu kwa mwaka ni asilimia
2.5, hivyo makadilio ya idadi ya watu mwaka 2015 ni 218,952 kati ya hao wanaume
ni 103,484 na wanawake ni 115,468
Kiuwakilishi Jimbo hilo linawakilishwa na Mbunge Dkt Emmanuel Nchimbi ambaye amekuwa mwakilishi
kwa kipindi cha miaka 10 na juni 22 mwaka huu ametangaza kutogombea tena jimbo
hilo lenye kata 21 ambapo kati ya hizo Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema lina madiwani 6 na chama cha mapinduzi kina madiwani 15
Kama yalivyo majimbo mengine nchini mwaka huu yanasimamisha
wagombea kutoka kwenye vyama mbalimbali vya siasa ambazo vimesajiriwa na
kukidhi vigezo vilivyowekwa na mamlaka husika nchini na kwa mantiki hiyo Jimbo
la Songea mjini nalo linapita katika mchakato wa kugombewa na makada kutoka
kwenye vyama shindani hapa Songea Mjini
vya Chadema na Ccm
Ndani ya chama cha Demokrasi na Maendeleo
(CHADEMA)kimebahatika kuwapa fomu za kugombea ubunge jimbo la Songea mjini
makada wake watano akiwemo Joseph Lusius Fuime,ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti
wa Chadema Mkoa wa Ruvuma na sasa ni Diwani wa Kata ya mjini ,Fredrick Fussi,
Edson Mbogoro ambaye ni wakili msomi, Daktari Walter Ngonyani , mwingine ni
Mfamasia katika Hospital ya Mkoa wa Songea Mussa Abdallah Ndomba
Nimepata fursa ya kuzungumza mambo machache na kada Mussa Ndomba ambaye amechukua fomu na
kukamilisha taratibu zinazohusika na kuirudisha fomu hiyo ya kuomba kugombea
ubunge ndani ya chama chake ili aweze kuruhusiwa kugombea katika uchaguzi wa
octoba 25 mwaka huu
“Nimekusudia kuchukua fomu na kugombea nafasi hiyo nyeti
kutokana na msukumo wa dhati wa kutaka kukomesha ufisadi ndani ya Halmashauri,
kukuza biashara na kilimo, pia kuboresha huduma za kijamii kupitia kauli mbiu
yangu ya hakuna wa kutusaidia bali ni sisi wenyewe”alisema Ndomba
Alisema kuwa kumekuwa na usimamizi dhaifu wa bajeti, mali za
wananchi na maliasili zinazopatika ndani ya halmashauri ya manispaa ya songea,
hali hiyo inatokana na udhaifu wa viongozi waliopo ambao wanauelewa
mdogo,ukosefu wa dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi wao
Kushiriki vitendo vya rushwa na kutanguliza maslahi yao
binafsi hali ambayo inaifanya halmashauri hiyo iyumbe kutoa huduma stahiki kwa
wananchi wake na hilo linathibitishwa na taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa
hesabu za serikali(CAG) kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 na 2013/14
Taarifa hiyo ya mwaka 2012/13 imeonyesha mali za halmashauri
zilizo katika hatari ya kuliwa na wajanja wachache ni jumla ya Shs
3,048,093,251/= ikiwa na mchanganuo kama ufuatao kutokana
na ardhi na majengo ambayo ni mali ya halmashauri kutokuwepo kwa hati na
hazijulikani zilipo ni Tsh 3,045,587,251/=
Pia mkaguzi
ameainisha kiasi cha Tsh 2,506,000 ambacho kimetolewa bila kufuata utaratibu
kwani hazikupitishwa na mamlaka husika, hivyo ni jukumu la wakazi wote wa
Halmashauri ya Manispaa kuchukua hatua kwenye sanduku la kura mwaka huu
Inaon yesha wazi kuwa hakuna nidhamu ya matumizi katika
kusimamia bajeti kwani jumla ya Tsh 10,239,921 ambazo zilitumika tofauti na
malengo kusudiwa hali iloyosababisha jumla ya Tsh 955,927,713 zipotee na
kuambulia kupewa hati zenye mashaka
Kwa mwaka 2012/13 na 2013/14 pekee jumla ya Tsh
945,687,792/= zilikuwa na taarifa zenye utata zinazoashiria wizi mkubwa kwani
fedha hizo zilitengwa kwa ajili ya manunuzi ya madawa,ruzuku ya kuendeleza mji,ruzuku
ya maendeleo na mambo mengine
Kumekuwepo na ufisadi na ubadhirifu mkubwa sana kwani katika
kaguzi za miaka hiyo miwili ya fdedha
zilizopita kiasi cha jumla ya Tsh 29,848,525,684/= hazijatolewa ufafanuzi hali
hiyo ni lazima ikomeshwe kwani haikubaliki na wahanga wakubwa wa uzembe huo ni
wananchi ambao kimsingi ndio walipa kodi
Ndio maana kauli mbiu inayofaa katika kipindi hiki kigumu ni
hakuna wa kutusaidia katika kuondokana na ufisadi huo bali ni sisi wenyewe kwa
kuchagua viongozi wenye uchungu na wazalendo wa kubwa wa jimbo hili la songea
Kwani kumekuwa na udhaifu katika kubuni vyanzo vipya vya
mapato na kusimamia vyanzo vilivyopo kutokana mikataba mibovu iliyosainiwa na
mawakala wa ukusanyaji wa mapato hali ambayo imesababisha mapato ya ndani kushuka
kwa kasi na kusababisha huduma kuwa duni
Taarifa ya CAG ya mwaka 2013/14 imeonyesha jumla ya Tsh
402,739,894/= hayakukusanywa kutokana na usimamizi dhaifu wa viongozi wa
Halmashauri kwani maeneo muhimu ya ushuru wa huduma za minara ya simu
haikukusanywa, ruzuku kwenye mitaa hazikuperekwa na kuwafanya wananchi
wachangie uendeshaji wa ofisi za mitaa na huduma zingine na kuwafanya waendelee
kuwa duni
“Suluhisho la Pekee ni kuwaondoa viongozi wanaowakandamiza
wananchi kwa kuwachangisha michango ya
fedha kwa lazima huku fedha
nyingi zinaliwa na wachache, fedha zingine za ruzuku zinarudishwa hazina huku
miradi haijaisha na wananchi wanaendelea kuchangishwa ovyo, sheria ya manunuzi
ya umma inavunjwa, hali hiyo inatakiwa kuikomesha na wakati wenyewe ni huu”alisema
Ndomba
Alisema uvunjwaji wa sheria kwa mwaka wa 2012/13 na 2013/14
kumesababisha matumizi mabaya ya kodi za wananchi na kuathiri maendeleo ya
wananchi katika jimbo la Songea mjini kwenye sekta zote na kulifanya jimbo hilo
kudumaa kuliko majimbo mengine yaliyopo mkoa wa Ruvuma
Alifafanua kuwa katika utafiti alioufanya na kuona mambo
ambayo yamepelekea kurudisha nyuma maendeleo ya wanasongea nimeamua kujitokeza
mbele ya wenzangu ili wanipe ridhaa ya kuyakomesha hayo kwa kufanya mambo yenye
ustawi stahiki
Wananchi wanatakiwa kuipumzisha Ccm na kuipigia kura Chadema
kwani ndio suluhisho pekee na sahihi kwani tumedhamiria kuwaongoza watanzania
katika kuyaondoa matatizo yanayowakabili na kuwapatia ustawi katika jamii zao
Kada huyo Ndomba alisema kuwa akifanikiwa kupata ridhaa
ndani ya chama chake na wananchi wajimbo la Songea kuchaguliwa kuwatumikia
pamoja na kutekeleza ilani ya chama
chake pia atajikita kuwatetea wafanyabiashara ndogondogo na wakulima
Alisema kuwa anatambua uwepo wa waendesha yeboyebo, wamachinga,
wafanyabiashara wa masoko na maduka, wakulima,mamalishe,wauza mitumba,waosha
magari, wasusi na vinyozi, na wengine
lakini wamekuwa wakikandamizwa sana na kanuni, sheria zinazotungwa na
Madiwani wa Halmashauri
Hivyo zikipatikana kanuni bora na kutengewa maeneo rafiki
kwa biashara zao ili waweze kurudisha mikopo waliyoanzishia biashara zao au
wakuze mitaji yao na kuifanya halmashauri kuwa rafiki kwa wananchi wake
Malengo yangu ni kuwatengea maeneo sahii na yenye wateja
kulingana na makundi ya biashara zao naamini tutazalisha ajira nyingi na
maendeleo ya mtu mmoja mmoja yatafikiwa na yataonekana na kuwafanya wawe na
uchumi imara na kuwawezesha kumudu kaya zinazowazunguka
Pia kuondoa ushuru,kodi zisizo na tija na michango
mbalimbali inayowakandamiza wananchi kwani kwa sasa fedha hizo zimekuwa kikwazo
kwa wananchi,kuna mapato mengi yanapotea kwenye vyazo vingine vya mapato hivyo
tutavibana hivyo na kubuni vyanzo vipya badala ya kuwakamua wafanyabiashara
ndogondogo
Nitahakikisha wajasiliamali wanapata mafunzo stahiki ya
majukumu yao na kuwatafutia taasisi za fedha zenye riba nafuu na kuyawezesha
makundi mbalimbali ya wajasiriamali ili waweze kukopeshwa kwa urahisi na waweze
kusaidiana katika jamii zao
Jambo jingine la muhimu ni kusimamia upatikanaji wa pembejeo
na utafutaji wa masoko ya mazao kwani kwa sasa mifumo yake ya upatikanaji
haisimamiwi vizuri, hivyo ni kipata fursa ya uwakilishi nitasimamia upatikanaji
wa pembejeo bora na kwa wakati pamoja na masoko ya kudumu ya mazao yao ili
waweze kufaidi kazi zinazotokana na kilimo
Nimedhamiria kuwatetea wachimbaji wadogowadogo wa madini na
wafanyabiashara ambao wanazunguka kwenye machimbo ya madini yaliyopo mkoani
Ruvuma kwani kumekuwepo na ukiukwaji wa haki za binadamu huko kwenye migodi
Katika suala la huduma ya afya natambua kuna matatizo mengi
lakini nimejipanga kikamilifu kudhibiti matumiza mabaya ya ruzuku ya vifaa vya
tiba na madawa yake na kuiladhimisha serikali kuunda mamlaka ya udhibiti wa bei
za madawa na vifaa vyake kama ilivyo Sumatra na Ewura lengo wananchi waweze
kunufaika na huduma ya afya
Katika huduma ya upatikanaji maji safi na salama, umeme wa
uhakika,miundombinu ya barabara na ujenzi wa madaraja, vivuko, usafi wa
mazingira, huduma za elimu, ardhi na upimaji wake,makundi yanayoishi katika
mazingira hatarishi na michezo
Nimezizingatia sana sekta hizo muhimu katika maendeleo ya
jamii na wananchi kiujumla hivyo nafahamu changamoto zinazozikabili sekta hizo
na kwamba nimeziwekea mikakati kabambe ya kukabiliana na changamoto husika
Jambo la muhimu ni kutambua haki ya kila mmoja katika
kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu hapo ifikapo Octoba25 ni lazima apatikana
kiongozi ambayo anazifahamu changamoto zinazowakabil;I wananchi wa Songea Mjini
na mikakati ya kuziondoa
Tumeona kuwa Jimbo hili toka nchi ipate uhuru lilikuwa
linaongozwa na Chama cha Mapinduzi lakini imefanikiwa kulifikisha hapo lilipo
kazi iliyobaki ni kulipatia mikononi mwa Upinzani ili tuweze kuamliza
changamoto ambazo zimeshinwa kumalizwa na Ccm
Kada huyo wa Chadema kabla ya kuomba kugombea ubunge amewahi
kufanya mambo mbalimbali ndani ya chama na jamii inayomzunguka kwa kujitolea na
kushirikisha wadau wa maendeleo, aliweza kufanikisha uchimbaji wa kisima cha
kupampu shule ya msingi Mitawa
Alitoa bati 40 kwa ajiri ya kuezekea jingo la zahanati
Sanangura,kupinga uporaji wa ardhi katika mtaa wa Mitawa,kupinga na kuongoza
mapambano dhidi ya ufisadi katika kata ya Tanga, kusaidia vifaa vya michezo kwa
timu 11 za mpira wa miguu za kata ya Tanga,kuchangia kikundi cha kwaya ya Tanga
kanisani na kufanikisha kurekodi albamu yao ya nyimbo za injili
Kukarabati choo shule ya Msingi Pambazuko katika Mtaa wa
mlete,kuweka sakafu katika vyumba vya madarasa shule ya msingi Mitawa,Kuleta
muhudumu wa zahanati ya Tanga(Peace Corp), kuwaunganisha watu wenye magonjwa
sugu na mradi wa uangalizi majumbani(HBC) na kuwapatia sare na vifaa vya shule
watoto 100 wa shule ya msingi MVC na mambo mengine mengi
Harakati za kisiasa alianza toka akiwa kidato cha tano
katika Sekondari ya kibiti mkoa wa Pwani mwaka mwaka mwaka 2002 na alipofikia elimu yake ya
juu alifanikiwa kupata cheti kutoka kwa Mwenyekiti wa Chadema Tawi la St.John’s University
of Tanzania kutokana na mikakati yake ya kiuongozi na kufanikisha harakati njema za chama
alifanikiwa kupewa cheti cha uongozi na
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe kwenye ukumbi wa polisi mesi Dodoma
Kielimu Mussa Ndomba ni Mfamasia na anafanya kazi hiyo
katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Songea, pia ni Mtaalamu wa masuala ya
usimamizi wa biashara hasa katika kada ya manunuzi, ni mwalimu na ni mtaalamu
wa masuala ya kibenki na huduma za mikopo
Kutokana na hayo machache nimejipima kuwa natosha
kupeperusha bendera ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Jimbo
la Songea Mjini hivyo naomba wanachama wenzangu mnichague ndani ya chama ili
niweze kuwa mgombea wa ubunge katika jimbo hilo
Ni muhimu kutanguliza maslahi ya wananchi kwanza kupitia
kauli mbiu mahususi kuwa hakuna wa kutusaidia kuondokana na ufisadi,
ubadhirifu,rushwa na ukandamizwaji mbalimbali wa haki za binadamu na kwenda
kwenye ustawi stahiki bali ni sisi wenyewe , tuanze sasa kubadilika kwani
tusisubili kesho kwani kesho haiwezi kufika bila kumaliza salama leo,
nimetafakari natosha kuwawakilisha, sote kwa pamojo tujikomboe
Mwandishi wa Makala haya
Anapatikana 0715-335051
www.mangokwetu.blogspot.com
Chapisha Maoni