WANACCM SONGEA MJINI WAONYWA UCHAGUZI WA 2015
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi (Ccm) Wilaya ya Songea
Mjini wametakiwa kuungana kwa pamoja na kuwa makini na vyama vya upinzani ili
kuhakikisha ushindi unapatikana kwenye kata tano ambazo zinashikiliwa na Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kati ya kata 21 za jimbo la Songea Mjini
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana baada ya kuchukua
fomu ya kugombea Udiwani wa Kata ya Mjini kupitia Ccm kwenye ukumbi wa mikutano
wa chama hicho kaya ya Mjini Shaibu Kitete alisema kuwa kuelekea kwenye
uchaguzi mkuu wa Udiwani,Ubunge na Urais wanaccm wanatakiwa kushirikiana ili
kuhakikisha ushindi unapatikana kwa kishindo
Kitete alisema kuwa kwenye uchaguzi uliopita wa Mwaka 2010
wanaccm hawakushirikiana ipasavyo ndio maana walipoteza majimbo mengi na kata
nyingi ikiwemo kwenye kata tano zilizopo
maeneo muhimu ya mjini za jimbo la
Songea Mjini na kufanya Ccm kushinda pembezoni mwa mji ambapo kwa kata hiyo kwa
sasa inashikiriwa na Joseph Fuime kupitia Chadema
Akieleza vipaumbele vyake vya kuomba kuchaguliwa na
wanachama wenzake kwenye kura za maoni na baadae kwenye uchaguzi mkuu ifikapo
Octoba 25 alisema kuwa anadhamira ya dhati ya kuirudisha kata hiyo ya mjini Ccm
kutoka Chadema na kwamba anaamini atawatumikia vyema wananchi wa kata hiyo kwa
kuhakikisha afya bora inapatikana kwa kuhakikisha kuwa dawa zote zinazoletwa na
Serikali zinatumika kwa lengo mahusisi na kwamba kuzuia vibali vya kujenga
maduka ya dawa karibu na zahanati na vituo vya afya ili kuzuia wizi wa dawa za
Serikali
Alisema kuwa kwa kushirikiana na Viongozi wenzake na Ilani
ya Uchaguzi ya Chama chake atahakikisha kuwa usafi katika kati ya mjini unakuwa
wa uhakika ili kuondokana na hofu ya miripuko ya magonjwa kwani maghuba
yamejengwa na wananchi wanatupa takataka zao lakini kumekuwa na utaratibu mbovu
wa kuzitoa taka hizo na kwenda kuzitupa mbali na mji
Alifafanua kuwa Sekta ya miundombinu nayo nimeiwekea mkazo
sana kwani ni jambo la aibu kwa kata ya Mjini licha ya kuwa ndio makao makuu ya
Mkoa wa Ruvuma lakini bado barabara zake nyingi hazina lami na kufanya mji kuwa
na vumbi kama kijijini
Kwenye sekta ya Elimu ndio chimbuko la ukombozi wa wanyonge
hivyo mkazo nimeweka kwenye kuongeza idadi ya mashimo ya vyoo, madarasa na
vifaa vya kujifunza, kufundishia na vifaa vya maabara kwenye shule zote za
Sekondari zilizopo kwenye kata ya Mjini
“Natambua pia changamoto za wafanyabiashara wadogo wadogo
kutokana na kanuni na shewria kandamizi ambazo zinatumika hivyo muda umefika wa
kushirikisha wadau na kuziondoa sheria hizo ambazo zimeonekana kandambizi ambazo
zimeendelea kuwanyanyasa na kuwafanya waendelee kuwas masikini ”Alisema Kitete
Alisema kuwa zipo changamoto zingine ambazo zimeendelea kuwa
kikwazo kwa maendeleo ya wananchi nitahakikisha naziondoa kwa muda mfupi ili
wananchi waifurahie halmashauri yao kwa kupata huduma bora za kijamii na
kiuchumI
MWISHO
Chapisha Maoni