Waziri wa Nchi Sera na Uratibu wa Bunge na ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama akisisistiza jambo kwenye moja ya Mikutano yake ya kisiasa Jimboni mwake
Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama akiserebuka na wapiga kura wake |
JENISTA MHANGAMA AMBAYE NI MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO AKIFUTURU JIMBONI MWAKE NA KATIBU WA CCM TAIFA ABRAHAM KINANA NA VIONGOZI WENGINE WAANDAMIZI WA CHAMA NA SERIKALI
NA STEPHANO MANGO, SONGEA,
WANANCHI wa kata ya Mkongotema na Madaba Wilaya ya Songea vijijini
Mkoa wa Ruvuma wamemchangia fedha taslimu kiasi cha sh.250,000/= mbunge wa
Jimbo la Peramiho na Waziri wa Nchi Sera
na Uratibu wa Bunge Jenista Mhagama ili
aende akachukue fomu ya kuwania tena nafasi ya ubunge kwenye jimbo hilo mwaka
huu wa uchaguzi.
Wananchi hao walimchangia fedha hizo jana wakati wa hafla
fupi ya ufunguzi wa ofisi ya Chama cha Mapinduzi Tawi la kijiji cha Mkongotema
baada ya kumaliza ziara yake ya siku kwenye Jimbo hilo ambapo Mbunge huyo Mhagama alikuwa
mgeni rasmi kwenye afla hiyo ambayo ilihudhuliwa na wananchi kutoka vijiji vya
jirani na kata hiyo pamoja na viongozi wa chama na serikali.
Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa ofisi hiyo ya CCM Tawi
mbele ya mgeni rasmi Diwani wa kata hiyo ya Mkongotema Vistus Mfwika alisema kuwa wananchi wa kata ya
Mkongotema na Madaba wameridhishwa na utendaji kazi wa mbunge huyo Jenista
kwani hadi sasa miradi mbalimbali ya maendeleo imetekelezwa kwenye kata zao
ikiwemo miradi ya maji na ujenzi wa zahanati jambo ambalo limewapunguzia
wananchi kwa kiasi kikubwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo muhimu
Mfikwa alisema kuwa wananchi hao ambao wanategemea kupata
kipato chao kwa kutegemea kilimo cha tangawizi,alizeti na mifugo wameamua kwa
moyo wa dhati kuchangia fedha hizo taslimu kiasi cha sh 250,000 ili aridhie tena
kwenda kuchukuwa fomu na kwamba wananchi bado wanaimani nae.
“Mheshimiwa Mbunge wananchi hawa unaowaona mbele yako wamejitolea bila kushinikizwa na mtu yeyote
kutokana na utendaji wako wa kazi hivyo hawaoni sababu ya kuhangaika kwa kumchagua mtu
mwingine zaidi yako na kama yupo basi asahau kabisa kuwa wanamkongotema na
Madaba hawatampa kura pindi uchaguzi utakapofika oktoba mwaka huu.”alisema
Mfikwa.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa
Sera Uratibu na Bunge,na mbunge pekee mwanamke katika Mkoa wa Ruvuma, alisema
kuwa anawashukuru wananchi hao kwa kuonesha kuwa na imani nae na kwamba CCM chini
ya uongozi wa Rais wa Jamhuri wa Muungano Dkt. Jakaya Kikwete imefanya mambo
mengi na hiyo yote ni utekelezaji wa ilani ya chama hicho.
Mhagama alisema kuwa changamoto ni nyingi lakini CCM
imejitahidi kuzifanyia kazi hasa kwenye maeneo ya Barabara,maji,umeme na afya
na kwamba pamoja na utekelezaji huo wa kuboresha miundo mbinu wapo watu kazi
yao ni kuwabeza viongozi wa CCM jambo ambalo amesema kuwa si la kiungwana kwani
mnyonge mnyongeni haki yake mpeni sio kila siku kusifia mabaya tu.
MWISHO.
Chapisha Maoni