NA STEPHANO MANGO,SONGEA
JUNI
22 ni siku ya historia kwa wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Songea ikiwa ni siku moja nyuma baada ya mbunge wa Monduli na Waziri
Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kufika Songea na kudhaminiwa na wanachama wa
chama cha mapinduzi (Ccm) mkoa wa Ruvuma zaidi ya elfu 52, Mbunge wa
Jimbo la Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi aliwaacha njia panda wapiga
kura wake na kuwafanya walie kwa kutoamini baada ya kuwaaga na kusita kuwakubalia wananchi wa jimbo la nyasa ambao wanamtaka agombee jimbo hilo
Mbunge
huyo Nchimbi akizungumza na viongozi wa mashina, matawi, kata
,madiwani,wenyeviti wa mitaa, mabalozi na wa Wilaya ya Songea mjini
kwenye uwanja wa michezo wa Majimaji mjini hapa alisema ni ukweli
uliowazi kuwa tumepata mafanikio makubwa katika maendeleo ya jimbo
kwenye sekta ya elimu,maji,afya,barabara na ujenzi,kilimo na
ushirika,mifugo na uvuvi,ardhi na maliasili,umeme,mawasiliano,biashara
na masoko,utawala bora na michezo
Lengo
la mkutano wake ilikuwa ni kuwaeleza wapiga kura wake taarifa ya
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Ccm kwa kipindi cha miaka 10 ambayo
yeye akiwa mbunge alikuwa mwakilishi wao alisema mambo mengi ambayo
nakusudia kuyaainisha katika makala haya ili niweze kuwafumbua macho
watanzania juu ya sababu zilizowaliza wananchi wa songea kufikia hatua
ya kumsihi na kumshawishi agombea tena ubunge katika jimbo husika.
“Nimepongezwa
sana kwa mafanikio makubwa tuliyoyapa lakini naomba nikiri wazi kuwa
kazi hizi sikuzifanya peke yangu, hivyo kwa heshima kubwa naomba
niwashukuru nyie viongozi wenzangu wa chama na serikali mliopo hapa na
wale ambao wamepita ndani ya miaka hii kumi ya uongozi wangu kwani
walikuwa chachu ya maendeleo,hata hivyo sikusudii kugombea tena jimbo
la Songea” alisema Nchimbi
Alisema
kuwa katika kipindi hiko cha miaka kumi Jimbo la Songea Mjini lilipata
heshima kubwa sana kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete kwa kumuamini na
kumteua kushika Unaibu Uwaziri katika Wizara mbalimbali na baadae
uwaziri kamili katika wizara mbili tofauti lakini pia amekuwa chachu na
kimbilio langu wakati wote ambapo nilikwama katika kusukuma gurudumu la
maendeleo ya jimbo la Songea, hivyo namshukuru sana yeye binafsi na
serikali yake kwa imani na mapendo yake kwa wananchi wa Songea Mjini
Alisema
kuwa nimepata wakati mgumu sana kuyasema maneno haya lakini nimeyasema
kwani ilani na ahadi zangu binafsi nimezitekeleza kwa ukamilifu na nyie
wenyewe ni mashahidi kwani yote niliyoyasema hapa huko kwenye maeneo
yenu mnayaona hivyo nataka niondoke nikiwa kifua mbele
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti baadhi ya viongozi wachama na serikali siku hiyo
walionyesha masikitiko makubwa sana na maneno aliyoyasema Dkt Nchimbi
ambayo kisiasa yalionyesha kuwa ndio anawaaga kutogombea jimbo hilo
ingawa pia hajasema anakwenda wapi.
Wachambuzi
wengi walionyesha maoni yao kutokana na hatua hiyo ya Dkt Nchimbi na
kuitafsiri kwa kina na kueleza namna walivyochanganyiwa na kuwaacha hoi
huku wakiwa njia panda kutokana na kauli yake hiyo kwani wanaamini mchango wake kwa maendeleo ya jimbo hilo ni mkubwa sana.
Walimtaja
kuwa Dkt Nchimbi uongozi wake waliuzoea na hata alipokosea walimshauri
naye alijirekebisha sasa leo ghafla anatuacha na nani na huyo anayekuja
mpaka tutakapomzoea na kumsahihisha atakapokosea itakuwa kasi ya
maendeleo imesimama kwa muda mrefu
Ingawa awali
duru za kisiasa zilionyesha kuwa miongoni mwa makada vijana ambao
walikuwa wanatajwa sana kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais Dkt
Nchimbi alikuwa ni mmojawapo lakini mpaka leo hajajitokeza kuchukua fomu
ingawa taarifa zinasema ameamua kuwaunga mkono makada waliochukua fomu
kwani ana imani yupo Rais ajaye
Kutokana
na hilo nawajibika kuweka mambo machache ambayo wananchi wa jimbo la
Songea mjini wanamkumbuka na kumlilia na wengine kumtaka arudi tena
kugombea jimbo hilo na hasa baada ya kuwafanyia mambo makubwa katika
kipindi cha miaka kumi yaani 2005-2015 katika sekta mbalimbali
Na
kwa kuanzia najaribu kumulika sekta ya elimu toka mwaka 2005 mpaka sasa
kwani kwa elimu ya awali madarasa yalikuwa 45 na sasa yapo 77 na
uandikishaji umeongezeka toka watoto 2408 hadi watoto 4103 mwaka huu na
kwamba walimu wao wameongezeka toka 45 hadi 79
Elimu
ya msingi nayo kulikuwa na shule 62 za serikali 60 na binafsi 2 lakini
mwaka huu kuna shule 78 ambapo za serikali ni 73 na binasfi 5,
uandikishaji wa wanafunzi darasa la kwanza ulikuwa ni 4106 lakini sasa
ni 5731
Idadi
ya walimu shule za msingi imeongezeka toka walimu 737 hadi 1086 na
nyumba zao zilikuwa 85 na leo zipo 145 na hata madarasa yameongezeka
toka 465 na sasa yapo 648 ambapo ufaulu wao awali ilikuwa ni 1110 na
sasa imefikia 2584
Kwa
elimu hiyo ya msingi jitihada za kudhibiti mimba imefanikiwa kwani
ilikuwa mimba 2 hadi mimba 0 kutokana na ushirikiano wa wazazi, walimu
na wadau wengine wa elimu, na kwamba kwa elimu ya sekondari idadi ya
shule zilikuwa ni 8 lakini mwaka huu zipo 40
Ambapo
kidato cha nne na tano zilikuwa 4 na leo Nchimbi anaondoka kukiwa na
shule 7 ambapo wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza ilikuwa 1275 na
leo 2584 na kwamba idadi ya walimu ilikuwa ni 106 na leo ni 849
Walimu
wa masomo ya sayansi walikuwa ni 70 leo wapo 102 na nyumba za walimu
zilikuwa 70 na zimeongezeka mpaka 78 na idadi za vyumba vya madarasa
katika Sekondari zilikuwa ni 61 na kufikia 229, kwa upande wa maabara ya sayansi zilikuwa 7 na kufikia 26, na maktaba zilikuwa 2 na kufikia 4
Pamoja
na hayo ujenzi wa Shule ya sekondari ya Dr Emmanuel Nchimbi Kidato cha
tano na sita ambayo ameijenga mwenyewe kwa gharama ya shilingi milioni
mia moja na kumi na mbili elfu ikiwa ni mchango wake muhimu katika
kukuza elimu ikiwa ni ongezeko la mchango wake wa kutoa mabati katika
sekondari za kata zote 21 ni jambo ambalo limewaliza wananchi wengi
kwani alitoa mchango wa mabati 5480 na kofia 2500 vyote vikiwa na
thamani ya zaidi ya milioni 103,418000
Katika
miradi ya maji imetekelezwa kwa kasi na kufanya jumla ya zaidi ya
bilioni 40 na kuwafanya wananchi zaidi ya 218952 kutumia maji safi na
salama toka 2005 hadi 2015 kwani kiwango cha upatikanaji wa maji
umeongezeka kwenye maeneo ya pembezoni toka asilimia 23 hadi asilimia
46.6
Visima
virefu vya pampu vilikuwa viwili leo vipo 41, ambapo visima vifupiu
vilikuwa 99 na kuongezeka hadi 118 na hata kamati zake zilikuwa 5 na leo
zimefika 25 na jumuia zake za watumiaji wa maji zilikuwa 0 na leo
zimefikia 10, mifuko ya maji ilikuwa 5 na zimefikia 10 na vituo vya maji
mtiririko vimeongezeka toka 12 hadi 45
Katika
Sekta ya afya ununuzi alioufanya Dkt Nchimbi wa gari ya wagonjwa ya
kituo cha afya ni ushaidi tosha wa huduma ya afya kuwa njema kwani
umepunguza vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka
5 toka 581 hadi 298 kwa kila watoto 1000 waliozaliwa hai na zahanati
zimeongezeka kutoka 15 hadi 29, vituo vya afya vilikuwa viwili mpaka vitatu
Upatikanaji wa chanjo kwa watoto wadogo imeongezeka toka 4200
hadi 71740 na hata usafi wa mji nao umekuwa wa uhakika kwani kamatio
zimeundwa za usafi wa mji katika mitaa na malori mawili yamenunuliwa na
upatikanaji wa dawa za maambukizi ya virusi vya ukimwi, vituo vyake
vimekuwa vingi na huduma inapatikana
Maambukizi
ya ukimwi yalikuwa 15% mwaka 2005 na leo yapo 4%, wagonjwa wagonjwa
matibabu ya dawa za ARVs wameongezeka kutoka 0 hadi 9487 na vikundi vya
kuchukulia dawa vilikuwa viwili na leo vipo 15 na vituo ambavyo watu
wanaoishi na ukimwi vilikuwa vitatu
lakini jitihada za Nchimbi vituo hivyo vimefika 34 na wamefanikiwa
kupata jumla ya shilingi 29,770,000 ili kuviendeleza vikundi hivyo
kiuchumi
Vituo
vya ushauri nasaha vimeongezeka toka 3 na kufikia 25 na huduma za
kuzuia maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto nayo imefanikiwa kwani
ilikuwa ni 0 mpaka 24 na kwamba hata huduma za wagonjwa majumbani
ilikuwa ni vituo 8 na kufikia 18
Mtandao
wa Sekta ya barabara umeongezeka toka km 241.9 hadi kufikia 341.2
ambapo barabara za udongo nazo zimeongezeka toka 197.9 hadi 11.1 na
kwamba za changarawe zilikuwa km 40 na kufikia 115.4 na za lami zilikuwa
km 4 hadi kufikia 14.8 na madaraja yalikuwa 33 mpaka kufikia 67 na
kwamba makalvet wakati nchimbi anaingia mwaka 2005 yalikuwa ni 150 leo
anawaaga wapiga kura wake anawaachia makalvet 347
Ni
ukweli ulio wazi kutokana na utekelezaji wa ilani yake Dkt Emmanuel
Nchimbi toka 2005 hadi mwaka 2015 ikiwa ni miaka 10 ya uwakilishi wake
ni muhimu kutafakari upya siasa za songea mjini, ingawa nakusudia kuweka
wazi mafanikio yake katika sekta kumi na tatu zilizobaki katika
muendelezo wa makala haya
Ni
lazima niweka mafanikio yake katika sekta za kilimo na ushirika, mifugo
na uvuvi,ardhi na maliasili,umeme,mawasiliano,biashara na
masoko,utawala bora na michezo ili wananchi wapate fursa ya kutafakari
kwa kina mchango na uwakilishi wake kwa jimbo la Songea mjini katika miaka hiyo kumi am,bayo imesababisha wananchi hao walie pale alipowaaga katika uwanja wa michezo wa majimaji siku ya juni 22 mwa huu
Sote
kwa pamoja tushirikishane kwa kutoa maoni stahiki ambayo yataleta
matokeo kwa amaendeleo ya jimbo hili kwa vipindi vingine vijavyo huku
tukiyaenzi kwa busara mafanikio yaliyopatikana katika miaka kumi
iliyopita, nawakaribisha katika makala yangu ijayo ya mwisho ya kueleza
kilichowaliza wananchi wa Songea mjini kwa Mbunge wao DSkt Emmanuel
Nchimbi
Mwandishi wa Makala haya
Anapatikana kwa 0755-335051
Chapisha Maoni