RPC RUVUMA MIHAYO MSIKHELA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Na Stephano Mango, Songea
MWANAFUNZI wa mwaka wa pili wa chuo
kikuu cha St. Joseph tawi la songea Mkoani Ruvuma Emmanuel Peter Lunguya (25)
amekutwa chumbani kwake amekufa naada ya kujinyonga kwa kutumia kamba za viatu
zilizokuwa zimefungwa kwenye kenchi la paa ndani ya chumba alichokuwa amepanga.
Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimezibitishwa na kamanda
wapolisi wa Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela zimesema kuwa tukio hilo limetokea
juzi majira ya saa kumi ya jioni huko katika eneo la ruhuwiko karibu na shule
ya msingi Manispaa ya Songea.
Kamanda Msikhela alifafanua kuwa
inadaiwa siku hiyo ya tukio Lunguya alikutwa chumbani kwake akiwa ananing’inia baada
ya kujinyonga na majiranni walioshituka baada ya kuto onekana kwa siku mbili.
Alisema kuwa taarifa zaidi juu ya tukio
hilo zinadai kuwa mara ya mwisho Lunguya alionekana chuoni kwake Julai 29 mwaka
huu na siku ya alhamis ya wiki iliyopita alionekana akiwa hana tatizo lolote la
kiafya licha ya kuwa kwa siku za nyuma aliwai kulazwa katika hospitali ya
serikali ya mkoa Songea kwa muda wa wiki mbili na baadaye aliruhusiwa kurudi
nyumbani.
Alisema kuwa Lunguya inadaiwa alilazwa
katika hospitali hiyo baada ya kusumbuliwa na ugonywa wa akili ambao ndio
uliokuwa unamsumbua kabda ya mahuti kumkuta.
Alieleza zaidi kuwa askali polisi wa
idala ya upelelezi walifanikiwa kufika kwenye eneo la tukio ambako marehemu
alikuwa akiishi na walifanya uchunguzi wa awali wakishilikiana na mganga wa
hospitali ya serikali ya mkoa huo na kubaini kuwa Lunguya alijinyonga kwa zaidi
ya siku tatu zilizopita kwani mwili wa
marehemu huyo ulianza kuharibika.
Alisema kuwa Lunguya hakuna ujumbe
wowote alio uwaacha kabdala ajachua uamuzi wa kujinyonga na pia hakuna mtu yeyote anayehusishwa na tukio
hilo licha ya kuwa polisi inaendelea kufanya uchunguzi zaidi ya tukio hilo.
Mwisho.

Chapisha Maoni