0

               Kadi wa CCM Ruvuma Hamis Abdalah Ally
NA STEPHANO MANGO,SONGEA

KADA  wa chama cha mapinduzi CCM  wilaya ya Songea mjini mkoani Ruvuma ,Hamis Abdalah Ally amewataka baadhi ya vijana wa wilaya hiyo  kuachana na tabia ya kuwashabikia wagombea ambao wanaotaka kuligawa taifa kwa ukabila ,udini na ukanda .

 Wito huo ameutoa jana wakati akiwanadi wagombea wa CCM kuanzia ngazi ya Urais ,Ubunge na Udiwani katika mkutano wa kampeni uliyofanyika kata ya Mshangano iliyopo ndani ya jimbo hilo huku mamia ya wakazi wa eneo hilo walihudhuria.

 Hamisi alisema kuwa maeneo mbalimbali ambayo vijana walitumia kuwapata viongozi kwa kufanya ushabiki  yamekuwa na majuto makubwa kwa kuwa yaliweza kuwagawa na kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa na hatimaye kukatokea vurugu za wenyewe kwa wenyewe.

 Alisema kuwa inasikitisha sana kuona baadhi ya vijana wanapewa pombe aina ya viroba pamoja na kutiliwa mafuta lita mbili kwenye pikipiki zao kisha kuanza kutumika na wagombea hao bila kujali uhai wao jambo ambalo limesababisha baadhi yao kupoteza maisha na wengine wamepata ulemavu wa kudumu.

 “Vijana mnakurupuka na kuwashangilia wa gombea bila kutambua sifa zao sasa ni vyema mkatuliza vichwa vyenu mnapofikia kufanya maamuzi ya hatima ya kumpata kiongozi wa taifa ,jimbo na kata kwa kuchagua kiongozi aliye sahihi na mwenye maono  ya kweli ya kulitumikia taifa”alisema kada huyo Hamisi Abdalah Ally.

Kwa upande wake mgombea ubunge kwa tiketi  ya CCM jimbo la Songea mjini Leonidas Gama akiongea na mamia hao alisema kuwa kiongozi anapatikana kwa kupimwa kutokana na sifa zake za utendaji kazi na siyo kutumia ushabiki usiyo na maana.

Alisema kuwa unaweza kujaribu nguo dukani kama inakutosha lakini huwezi  kumjaribu kiongozi bali inatakiwa umpime kwa kina kwa kuangalia mwenendo na tabia zake ikiwemo na hoja  ambazo anazo wajengea wananchi.
 
MWISHO.

Chapisha Maoni

 
Top