NESTORY MWANJA |
MGOMBEA UDIWANI KATA YA MAPOSENI JIMBO LA PERAMIHO NESTORY MWANJA |
KATA ya Maposeni ina vijiji viwili vya Mdunduaro na Kijiji
cha Maposeni ni miongoni mwa kata 16 za jimbo la uchaguzi la Peramiho lililopo
katika Wilaya ya Songea Vijijini ambalo linagombewa na Jenista Mhagama kupitia
chama cha Mapinduzi na kwamba Kata hiyo kwa upande wa Udiwani inagombewa na
Nestori Mwanja
Kama zilivyo Kata zingine hapa nchini Tanzania zipo kwenye
hekaheka za kusikiliza sera za wagombea ili mara ifikapo Octoba 25 mwaka huu
waweze kuwachagua viongozi wenye nia thabiti ya kushirikiana nao katika
kukabiliana na changamoto zinazohusika kwenye maeneo yao
Kwani ni siku chache zimebaki za kufanya maamuzi sahihi
kupitia sanduku la kura na kufanya wawakilishi kupatikana ambao tutawajibika
kushirikiana nao katika ujenzi wa taifa letu kwa kipindi cha miaka mitano kama
inavyopaswa kwa mujibu wa katiba yetu ya Tanzania
Tutambue kuwa tukichagua kiongozi ambaye ana upeo mdogo wa
kufikiri, kutenda,kuamua,kuthubutu na kubuni atachangia kwa kiasi kikubwa
kurudisha nyuma guruduma la maendeleo, badala ya kulipeleka mbele kama
inavyotakiwa
Kwa mantiki hiyo nimevutwa na kauli mbiu ya Mgombea Udiwani
wa Kata ya Maposeni kupitia chama cha Mapinduzi( Ccm) Nestory Mwanja inayosomeka
“Maposeni Inataka Maendeleo Sasa” ambayo wapiga
kura wake wanafarijika kuisoma na kuiimba mara kwa mara kwenye mikutano yake ya
kampeni ya kuwaomba kura ili wamchague awe Diwani wa Kata hiyo kwa mwaka
2015-2020
Kada huyo maarufu wa Ccm Wilaya ya Songea na Mkoa wa Ruvuma
kiujumla aliwahi kushika nyadhifa
mbalimbali ndani ya chama hicho ambazo zinamfanya aonekane kuwa ameandaliwa
kuwa kiongozi amewahi kuwa Katibu wa Chipukizi na Mhamasishaji wa Uvccm Kata ,
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Ccm Wilaya
Aliwahi kuwa Katibu wa Chipukizi na Mhamasishaji wa Uvccm
Wilaya ya Songea na pia amewahi kuwa kiongozi wa mbio za Bendara ya Ccm Mkoa wa
Ruvuma na sasa anajitokeza mbele ya wananchi kuomba kura za kuwa Diwani wa Kata
ya Maposeni kwani amejipima na amejiona anatosha kuwa mwakilishi wao
“Hayo yote yatawezekana katika Uongozi wangu ikiwa
nitashirikiana na Wananchi kwa kuyapokea mawazo yao , kushirikiana nao na
kuyafanyia kazi kwani kwa pamoja tutaijenga Maposeni yetu kwa haraka zaidi”
ndivyo alivyoanza kuelezea maana ya kauli mbiu hiyo Nestory Mwanja
Mwanja alisema kuwa anatambua matatizo ambayo yapo kwenye
kata hiyo yenye Vijiji viwili vya Mdunduaro na Maposeni kwenye sekta ya
Utawala, Elimu, Afya, Maji, Uchumi, Miundombinu, michezo na Utalii
Hivyo amejitokeza kwa dhati kuomba kura kwa wananchi wenzake
ili waweze kumchagua ifikapo Octoba 25 mwaka huu awe mwakilishi wa kata hiyo
ili aweze kushirikiana nao kutatua changamoto husika kwenye kata hiyo
Akizungumzia changamoto hizo Nestory Mwanja alisema kwa upande wa elimu kwenye kata hiyo kuna
shule tatu za elimu ya Msingi kwa maana ya shule ya msingi Namakinga na Maposeni zilizopo kijiji cha
Maposeni na Kijiji cha Mdundualo kuna shule ya Msingi Ndirima na kwa upande wa
Sekondari zipo mbili moja ya mtu binafsi inaitwa Pehisco na ya Serikali inaitwa
Daraja Mbili
Mwanja alisema kuwa shule hizo za msingi na Sekondari
zinakabiliwa na ikama ya walimu, vifaa vya kujifunzia na kufundishia, matundu
ya vyoo na nyumba za walimu, hivyo mara atakapochaguliwa atahakikisha
anashirikiana na wadau muhimu wa elimu kukomesha hali hiyo
Alifafanua kuwa awali Maposeni ilikuwa ni makao makuu ya
Tarafa ya Ruvuma na ni makao makuu ya kata ya Maposeni, hivyo kulikuwa na
nyumba tisa za wafanyakazi ambazo zimechakaa na kufanya kuwa magofu hali iliyopelekea
watumishi kukwepa kuishi nyumba hizo na kuzitelekeza
Alisema kwa upande wa upatikanaji wa maji sio wa uhakika
hivyo akichaguliwa atashirikiana na Halmashauri na wananchi kuweza kutega
vizuri na kukihifadhi chanjo cha maji kilichopo kijiji cha Parangu ili kiweze
kutoa huduma ya maji kwenye kata ya Maposeni
“Wananchi walijitahidi kuchimba mitaro na kutandika mabomba
ili waweze kupata maji lakini wataalamu wa maji na ujenzi walishindwa kutimiza
wajibu wao wa kujenga vizuri chanzo hicho na kusababisha adha ya maji kuendelea
kuwepo, hivyo nikichaguliwa nitasimamia upatikanaji wa maji kwani vifaa vya
viwandani vipo” alisema Mwanja
Katika suala la afya kijiji cha Maposeni kuna Zahanati
ambayo ipo makao makuu ya kata inachangamo ya wahudumu, madawa na vifaa vya
tiba, lakini katika kijiji cha Mdunduaro hakuna Zahanati, hivyo nikipata
uwakilishi nitaisimamia vizuri Ilani ya Ccm kwa mwaka 2015-2020 ili kuboresha
huduma ya afya kama ilivyoelekezwa
Suala la miundombinu ya barabara ya kuunganisha vijiji ni
kero kubwa kwa wananchi, hivyo nitashirikana na Serikali kupata fedha za miradi
ya barabara kuhakikisha barabara ya kutoka kijiji cha
Maposeni kwenda kijiji
cha Nakahuga, kutoka kijiji cha Maposeni kwenda kijiji cha Morogoro zinapitika
na Daraja la Mto Likwambi ambalo linavusha wananchi kwenda Kijiji cha Kihurungi
kata mpya ya Parangu linajengwa kikamilifu
“ Zipo barabara zingine wakati wa mvua hazipitiki kutokana
na kujengwa kwa tope ambalo sio rafiki na hawajaweka changarawe, hivyo
nitahakikisha barabara hizo zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka ili wananchi
waweze kunufaika na hudumu zinazotolewa na halmashauri yao” alisema Mwanja
Changamoto nyingine inayoikabili kata hiyo ni migogoro ya
ardhi(mipaka) hasa katika kitongoji cha Mkingazi kilichopo Kijiji cha Mdunduaro
wananchi wamekuwa wakilalamika sana ardhi yao kuvamiwa na Kijiji cha
Muunganozomba kilichopo kata ya Kilagano, hivyo mara baada ya kuchaguliwa
nitawakutanisha wazee, viongozi wa serikali na wataalamu wa ardhi ili waweze
kutatua changamoto hiyo
Tatizo jingine linalowakabili wananchi wa kata hiyo ni mfumo
mbovu wa ugawaji wa pembejeo, ninawaahidi wakulima wa kata hiyo kutowaangusha
katika kusimamia ilani ya chama na kwamba viongozi wa vijiji na vitogoji
hawatakuwa na nafasi tena ya kuchakachua pembejeo husika
Alisema kuwa kwenye kata hiyo kuna tishio la imani za
kishirikina miongoni mwa jamii zake hali ambayo inaleta hofu kwa baadhi ya
wakazi wake, hivyo nitahakikisha elimu stahiki ya kupinga vitendo hivyo
inatolewa kwa ukamilifu ili wananchi waweze kuishi salama
Kwenye sekta ya nishati ya umeme nitapigania nishati hiyo
muhimi kiuchumi inafika kwenye kata hiyo mapema ili wajasiriamali na wananchi
waweze kunufaika na huduma muhimu ya upatikanaji wa umeme , kwani wananchi hao
wamekuwa wakiteseka sana kwani bila umeme kamwe hakuna nuru imara ya uchumi
“Nitajitahidi kupigania kupata fedha za miradi nikishirikiana
na mgombea ubunge makini Jenista Mhagama
ambaye naamini kwa namna
alivyowatumikia wananchi wa jimbo la Peramihoi atachaguliwa tena , ili vikundi tukavyovihamasisha kwa pamoja vya vijana na wanawake viweze kunufaika na wanavikundi hao waondokane na umaskini
uliokithiri miongoni mwao” alisema Mwanja
Alifafanua kuwa mikakati yangu ya kufanikisha hayo ipo
vizuri, ninachosubiri wananchi wanipe ridhaa ya kuniona, kunichagua ili
niwatumikie kwani maandalizi ya kutafuta fedha za kufanikisha utekelezaji wa
ahadi zangu binafsi yamekamilika kutoka kwa marafiki zangu na wananchi wenye
asili ya maposeni ambao hawaishi Maposeni na wadau muhimu wa maendeleo ya Maposeni
Naamini yote hayo yatawezekana ikiwa wananchi watatimiza
wajibu wao muhimu wa kunichagua na mara baada ya kunichagua wakatumia fursa
mbalimbali za kujipatia maendeleo kwa kuijenga maposeni kwa akili, utashi,
ubunifu na maarifa stahiki
Uchaguzi ni muhimu sana katika kumpata kiongozi bora kwenye
ngazi ya Urais,Ubunge na Udiwani hivyo tukiuharibu au kuukosea kwa ushabiki
tutapoteza nia ya dhati ya Serikali inayotokana na Ccm kwani ndio chama pekee
ambacho kina malengo stahiki ya kuwakomboa watanzania
Katika hili nawasihi watanzania tusikate tamaa na kubaki tukiangalia
makosa ya nyuma tu, bali tuangalie mbele kwa matumaini makubwa, hivyo tuamke na
kuanza upya kwani lawama haijengi ghorofa bali ghorofa linajengwa kwa misingi
imara, na uwajibikaji ndio unao leta mabadiliko imara
Nasi tunaweza kwa kupitia sanduku la kura Octoba 25 kwa
kuwachagua wagombea wanaotokana na chama cha Mapinduzi ili waweze kushirikiana
na wananchi kutatua changamoto zinazowakabili kwenye maeneo yenu
Taifa linahitaji viongozi makini kwa sasa ambao watawawezesha kuwaonyesha njia
wananchi wake ya kuyafikia maendeleo kwa kuzingatia vipaumbele kusudiwa, kwani
bila hivyo tutakuwa tukiharibu kwa makusudi mustakabali wa Taifa letu
Mwandishi wa Makala
Anapatikana 0715-335051
www.mangokwetu.blogspot.com
Chapisha Maoni