NA STEPHANO MANGO,SONGEA
CHAMA cha Mapinduzi katika jimbo la Songea Mjini Mkoani
Ruvuma Kimefanikiwa kuibuka ushindi wa ubunge baada ya kuhesabu kura mara mbili
na kumfanya mgombea wa chama hicho Leonidas Gama kutangazwa mshindi na
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Jimbo
hilo Rafael Kimari alisema kuwa kulikuwa na vyama vitatu ambavyo vilisimamisha
wagombea kikiwemo chama cha ACT WAZALENDO,CCM na Chadema
Kimari alimtangaza Leonidas Gama kuwa mshindi kwa kupata
kura 40,886, na kufuatiwa na mgombea wa Chadema Joseph Fuime aliyepata 37000 na
wa mwisho ni mgombea wa ACT WAZALENDO Emmanuel Msabila ambaye alipata kura 436
Alieleza kuwa katika jimbo hilo idadi ya waliojiandikisha
walikuwa ni wapigakura 127738 ambao walitakiwa kupiga kura zao 324 katika jimbo
la uchaguzi wa jimbo hilo
Alieleza kuwa jimbo lenye kata 21 chama cha mapinduzi kimefanikiwa
kushinda kata 16 , chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefanikiwa
kushinda kata 4 na chama cha wananchi Cuf kimeshinda kata 1
Awali kabla ya kutangazwa matokeo hayo ya nafasi ya Ubunge
wananchi walijitokeza kwa wingi kwenye viunga vya Halmashauri ya Manispaa ya
Songea kwa lengo la kupata matokeo ambayo yalitakiwa kutangazwa majira ya saa
5:00 asubuhi mpaka saa 6:00 mchana kushindikana na kusababisha Jeshi la Polisi
kuwataka kutawanyika na wao kukaidi na kusababisha matomu ya machozi kutumika
kwa lengo la kuwatawanya
Aidha toka majira ya saa 8:00 mchana barabara zilifungwa na
Jeshi la Polisi kutoa amri ya kufunga maduka na biashara zote hali ambayo
ilisababisha taaruki kwa wakazi wa manispaa ya Songea
Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti
Kmanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa wafuasi wa chadema
walivumiliwa kwa muda mrefu wakifanya fujo na kuranda randa katikatika ya mji
wakishinikiza matokeo yatangazwe bila kufuata utaratibu hali ambayo ilailazimu
Askari kutumia mabomu kuwatanya na kupisha utangazaji wa matokeo hayo
MWISHO

Chapisha Maoni