MGOMBEA UDIWANI WA KATA YA BOMBAMBILI GOLDEN SANGA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA.
MWENYEKITI wa chama cha mpira wa miguu mkioani Ruvuma
[FARU]Golden Sanga ambaye pia anagombea Udiwani kwenye Kata ya Bombambili Manispaa ya Songea ameweka makubaliano na viongozi wenzake wa kwenye chama
hicho kuhakikisha wanasimamia mapato ya timu ya majimaji kikamilifu ili
kuiondoa timu hiyo kwenye wimbi la umasikini la kuwa omba omba.
Makubaliano hayo yamefanyika hivi karibuni wakati wa mkutano
mkuu wa mwaka wa mkoa huo ambao uliyokuwa ukijadili ajenda mbalimbali za
utekelezaji wa michezo pamoja na maeendeleo ya soka ndani ya mkoa huo.
Akifunga mkutano huo
Sanga alisema kuwa sasa imefikia mwisho kwa timu kongwe kama majimaji kushindwa
kujimdu kimapato na kuwa ombaomba jambo ambalo limekuwa likiwafunja mioyo
wachezaji pamoja na mashabiki wa timu hiyo.
Alisema kuwa kwa
kipindi kadhaa timu hiyo ilikuwa imeshuka daraja na sasa imepanda kuchezea
lingi kuu la Vodacom ambayo itanza
September 12 mwaka huu ,hivyo inatakiwa
kama chama mkoa kujipanga vilivyo namna ya kuhakikisha timu hiyo haiyumbi hasa
katika masuala ya kiuchumi.
Aidha alisema kuwa
chama hakitamvumilia kiongozi yeyote ambaye amepewa thamana ya kukaa milangoni
kwa lengo la kukusanya mapato ya viingilio na kujifanyia tofauti ya maelekezo kwa maana ya kuiba mapato hayo.
Hata hivyo aliwataka
viongozi wa soka ngazi za wilaya mkoani humo kuhakikisha wanajitahidi kuibua
vipaji vya wachezaji ili kutoka kwenye wilaya zao ili kufanikisha kukabiliana na changamoto mbalimbali
za upatikanaji wa wachezaji pindi timu kubwa zinapofanya usajili wa wachezaji.
MWISHO.
Chapisha Maoni