MGOMBEA ubunge kupitia chama cha ACT
wazalendo jimbo la Namtumbo Mkoa wa Ruvuma Haroun Mpangala amewahidi wananchi
wa jimbo la uchaguzi la namtumbo kuwa endapo watamchagua oktoba 25 mwaka huu
watamchagua na kumpa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha kuwa
atashugulikia kwa karibu miundombinu ya sekta ya afya kwa kuboresha zahanati,
vituo vya afya, hospitali na kuhakikisha kuwa magari ya wagonjwa yanapatika kwa
kipindi cha mwaka mzima.
Mbawala aliyasema hayo hivi karibuni
kwenye mikutano miwili tofauti iliyofanyika katika kijiji cha Lusewa na eneo la
Luwinga lililopa Namtumbo mjini wakati alipokuwa akijinadi kwa kuwaomba
wananchi wamchague kwenye mikutano ya kampeni ambayo ilihudhuliwa na watu
walifika kumsikiliza,
Aliema kuwa wilaya ya Namtumbo ipo
nyuma kimaendeleo hasa katika sekta ya afya ambayo imeonekana kuwa ni kero
kubwa kwa wananchi hivyo amewaomba wananchi wampe ridhaa ya kuwatumikia kama
mbunge wao na kwamba endapo atachaguliwa
atahakikisha kila kijiji kinakuwa na zahanati na makao makuu ya kata
vitajengwa vituo vya afya ilikupunguza usumbufu unaojitokeza pale wananchi
wakiwemo watoto na akina mama wajawazito wanapo umwa na kushindwa kutibiwa
kutokana na umbali ambako ziko zahanati na vituo vya afya.
Alifafanua kuwa wilaya ya Namtumbo
inavituo vya afya vichache ambavyo vinamagari ya kubebea wagonjwa lakini magari hayo yamekuwa yakifanya kazi ya kuwabeba
wakubwa waliopo makao makuu ya Hamashauri hivyo endapo atachaguliwa magari hayo
yatafanya mkazi ya kuwabeba wagonjwa tu na sio kutembelea vigogo.
Mbawala pia aliwaomba wananchi kuwa
ifikapo oktoba mwaka huu wamchague mgombea wa uraisi kupitia ACT wazalendo Anna
Mgwila na waogombea udiwani kupitia chama icho ili wameze kuleta maendeleo
yenye mipango yakinifu ya sera za chama hicho.
Kuhusu sekta ya elimu endapo atakuwa
mbunge atahakikisha kuwa shule zte za msingi ambazo hazina vyumba vya kutosha
vya madarasa vinafanyiwa matengenezo ikiwa ni pamoja na kupeleka madawati ya
kutosha kwa kila shule ya msingi tofauti na ilivyo sasa mbunge alieyekuwepo wa
CCM alishindwa kusimamia sekta hiyo ambayo idadi kubwa ya shule za msingi
wanafunzi wakiwa darasani wanakaa chini kutokana na uhaba wa madarasa na
madawati.
Alisema kuwa tatizo la ajira kwa vijana
wa wilaya hiyo muda mfupi tu baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge atashauriana na
wataalamu wa idara ya ushirika kwa lengo ya kuanzisha chama cha akiba na mikopo
cha jimbo la uchaguzi la wilaya ya namtumbo ili vijana wawezekupatiwa mikopo
ambayo itaweza kuwasaidia kwa kuwaongezea vipato vyao vya kila siku.
Alisema kuwa vujana wa wilaya hiyo pia
waapatiwa elimua ya kutosha ya ujasiliamali ili waweze kumudu kuendesha biashara
zao na kujiajili wao wenyewe badala ya kusubili ajira serikalini ambayo
walikuwa wakidanganywa na mbungea wa CCM.
MWISHO.
Chapisha Maoni