MWALIMU wa shule ya sekondari ya Msamala mansipaa ya Songea mkoani Ruvuma Henry Milinga(34)amekutwa akiwa amekufa na kutupwa kwenye mtaro huku kwenye paji lake la uso kukiwa na jeraha na pembeni mwa mwili wake kukiwa na vipande vya chupa vya bia.
Habari zilizopakana jana mjini Songea na kuthibitishwa na
kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela zimeeleza kuwa tukio hilo
limetokea Novemba 5 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi katika eneo la Nane nane
lililopo Msamala mjini Songea.
Habari zaidi zimefafanua kuwa inadaiwa kuwa siku hiyo ya
tukio hilo mkuu wa Polisi wa wilaya ya Songea alipokea taarifa kutoka kwa raia
wema kuwa huko katika eneo la Nane nane Msamala kuna mtu mmoja ameonekana akiwa
katika eneo la mtaro akiwa amepoteza fahamu ndipo juhudi za makusudi za polisi
kufika eneo la tukio zilipofanyika na baadaye kwenda kwenye eneo la tukio na
kumkuta mtu huyo akiwa ndani ya mtaro.
Kamanda Mskhela alieleza zaidi kuwa askari polisi wakiwa
kwenye eneo la tukio huku umati mkubwa uliofika kushuhudia ndiyo baadhi yao
waligundua kuwa mtu huyo aliyekuwa mtaroni kuwa ni mwalimu wa shuleya sekondari
ya Msamasla ndipo alipotafutwa mkuu wa shule hiyo ya sekondari Irine Chitinde
ambaye alithibitisha kuwa huyo ni mwalimu mwenzake na jina lake ni Henry
Milinga mkazi wa eneo la kwa Gasa.
Alisema kuwa baadaye walifanya jitihada za kumchukua na
kumkimbiza katikja hospitali ya serikali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo
mjini Songea ambako daktari alithibitisha kuwa Milinga alikuwa ameshafariki
dunia kutokana na jeraha lake la kwenye paji la uso.
Uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa Milinga katika
uhai wake alikuwa akipendelea kunywa katika baa maarufu ya Mtini iliyopo kati kati
ya Manispaa ya Songea na kuwa inahofiwa kuwa mauti yalimkuta wakati akiwa
anarudi nyumbani kwake licha ya kuwa polisi bado inaendelea kufanya uchunguzi
zaidi ili kubaini chanzo cha kifo chake.
Mwisho.

Chapisha Maoni