Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MWANAFUNZI wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Skill
Path iliyopo katika halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Fatuma Ally
(7) amekutwa akiwa amekufa baada ya kujining’iniza kwenye kamba ya manila
ambayo ilikuwa ikitumika kwa ajiri ya kuanikia nguo nje ya nyumba ya wazazi
wake
Akizungumza na gazeti hili jana ofisini kwake Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea Disemba
12 mwaka huu majira ya saa 5 asubuhi huko katika eneo la mtaa wa Making’inda katika kata ya Msamala mjini
hapa
Msikhela alisema kuwa inadaiwa siku ya tukio huko katika
mtaa wa Making’inda jeshi la Polisi lilipata taarifa kuwa kwenye eneo hilo kuna
tukio la mtoto kujinyonga nje ya nyumba ya wazazi wake ,baada ya kupata taarifa
hizo Askari Polisi wakiwa wameongozana na Mganga walienda kwenye eneo la tukio
Alisema kuwa Askari Polisi hao mara baada ya kufika katika
eneo la tukio walimkuta Fatuma ameshafariki dunia akiwa kwenye mti na shingoni
ana kamba aina ya manila ambayo ilikuwa ikitumika kwa ajiri ya kuanikia nguo
nyumbani kwao
Alifafanua kuwa inadaiwa kabla ya tukio hilo Fatuma alikuwa
akicheza kwenye kamba hiyo kama kawaida yake hali ambayo siku hiyo ilimsababisha
kujining’iniza na kupelekea kifo chake na kuleta mshangao mkubwa
Alieleza zaidi kuwa tukio hilo lilitokea wakati baba yake
mzazi Ally Omari ambaye ni Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kambi
ya Chandamari alipokuwa anakunywa chai huku mtoto wake Fatuma akiwa anacheza
nje ya nyumba hiyo kwenye kamba ya kuanikia nguo
Kamanda huyo alisema kuwa baba wa mtoto huyo baada ya
kumaliza kunywa chai alitoka nje na kumkuta mwanae akiwa amening’inia kwenye
moja ya kamba ya kuanikia nguo huku ulimi wake ukiwa nje
Alisema kuwa mwili wa marehemu Fatuma tayari umefanyiwa
uchunguzi wa kina na timu ya wataalamu wakiwemo Askari wa Idara ya Upelelezi na
Mganga wa Serikali ya Mkoa wa Songea na tayari umekabidhiwa kwa ndugu wa
marehemu kwa taratibu za mazishi na kwamba upelelezi zaidi wa tukio hilo
unaendelea
MWISHO
Chapisha Maoni