0
    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela

NA STEPHANO MANGO,SONGEA

NYUMBA 23 zimeezuriwa na upepo mkubwa ulioambatana na mvua kali huko katika Kijiji cha Magagura wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma na kusababisha Philibeta Komba (35) kujeruhiwa vibaya baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba yake

Akizungumza jana ofisini kwake na gazeti hili Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku huko katika kijiji cha Magagura ambapo wananchi walikumbwaq na maafa hayo

Msikhela alisema kuwa inadaiwa siku ya tukio mvua kubwa yenye kuambatana na upepo mkali kwenye kijiji hicho iliezua nyumba 23 ambapo kati ya hizo ni nyumba tisa zilianguka na kubomoka na kufanya kaya zilizokuwa zinaishi kwenye nyumba hizo kukosa mahali pa kujihifadhi na kuendelea kuishi

Alieleza kuwa katika tukio hilo Philibeta amejeruhiwa vibaya sana kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba yake na kwamba kwa sasa amelazwa katika Hospital ya Misheni ya Peramiho kwa ajiri ya matibabu zaidi

Aidha katika tukio linguine Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma nyumba 38 zimeezuliwa na upepo mkubwa ambao uliambatana na Mvua na kusababisha kaya zake kukosa mahali pa kuishi

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa za mchana huko katika Kata ya Luanda Wilayani Mbinga kwenye vijiji viwili tofauti ambako mvua kali iliyoambatana na upepo ilinyesha na kuezua nyumba hizo

Alifanua kuwa katika kijiji cha Luanda nyumba 14 ziliezuliwa na katika kijiji cha jilani cha kihuruku ziliezuliwa nyumba 24 na kufanya jumla ya nyumba zilizoezuliwa na upepo katika tukio hilo kuwa jumla ya nyumba 38 na kwamba mpaka sas hasara iliyopatikana kutokana na matukio hayo bado haijafahamika licha ya kuwa wataalamu tayari wameshaanza kufanya tathimini ya mahafa hayo
MWISHO

Chapisha Maoni

 
Top