0
KAMANDA WA POLISI RUVUMA ZUBERI MWOMBEJI

Na Stephano Mango,Songea

UCHAGUZI mkuu wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha St Joseph tawi la Songea mkoani Ruvuma umeshindwa kufanyika kwa madai kuwa uongozi wea chuo hicho umekuwa ukiingilia kwa kutaka kuweka uongozi wanaouhitaji wao jambo ambalo limesababisha kuwepo na vurugu ambazo zilipelekea mmoja wa viongozi wa chuo hicho ambaye ni mtawa Magadalena ambaye ni raia wa India amenusurika kipigo wakati anatangaza uchaguzi hauta fanyika.

Habari zaidi kutoka kwenye chuo hicho zimeeleza kuwa mapema miezi mitatu iliyopita wanafunzi wa chuo hicho baada ya uongozi wa serikali ya wanafunzi wa kipindi kilichopita muda wao kuisha walitangaziwa kuwa mwanachuo yeyote anayetaka uongozi achukue fomu ya kutaka kugombea.

  Wanachuo hao ambao waliomba majina yao yahifadhiwe waliwaambia waandishi wa habari kuwa baadaye mchakato wa kuwapata viongozi uliendelea ambapo wagombea walijitokeza kisha walianza kufanya kampeni za kuomba wachaguliwe kwa nafasi walizoomba.

Walisema kuwa siku chache kabla ya Februari tatu mwaka huu baadhi ya majina ya wagombea yalikatwa na uongozi wa chuo hicho na badala yake yaliletwa majina mengine ya wanachuo ambao hawakuomba nafasi hiyo jambo ambalo lilianza kuleta mgogoro baina ya wanachuo na uongozi wa chuo hicho ambao unatuhumiwa kuwapangia viongozi wa serikali ya wanachuo.

  Walifafanua kuwa siku ilipo wadia ya kufanya uchaguzi ya Februari tatu mwaka huu ndipo mtawa Magdalena aliitisha mkutano wa wanachuo wote na kuwatangazia kuwa uchaguzi wa serikali ya wanachuo umefutwa hadi pale watakapo tangaziwa na kuwa mchakato huo uanze upya ndipo vurugu zilipoanza.

“Mara baada ya kiongozi huo ambaye ni mtawa alipotangaza hivyo kuwa uchaguzi umefutwa wanachuo waliyowengi walishindwa kujizuia kwa malengo ya kutaka wapate ufafanuzi zaidi sababu za kufutwa kwa uchaguzi huo”walisema moja ya wanachuo hao.
 

Walisema kuwa kutokana na kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara kwenye chuo hicho baadhi ya wanachuo wameonyeshwa kusikitishwa kwa mwenendo wa uongozi wa chuo hicho ambao umekuwa ukisababisha kutokuwa na maelewano katika pande zote mbili na wameiomba serikali ya awamu ya tano kuona umhimu wa kuchukua hatua za haraka namna ya kumaliza migogoro inayojitokeza mara kwa mara chuoni hapo.

     Wanachuo waliyojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi zilizotangazwa kuwa ni kwa nafasi ya urais wa serikali ya wanafunzi iliwaniwa na John Zabron na Jonas Kawelela ,kwa upande wa makamu Urais waliyojitokeza kuwa ni George Ngao na Veronika Lusagira ambapo inadaiwa majina mawili ya wagombea yalikatwa na uongozi wa chuo na kuwa uongozi huo uliteuwa majina mawili mengine ili kujaza nafasi zilizokatwa jambo ambalo wanachuo waliendelea kulipinga.
 

Waliyokatwa majina kuwa ni Jonas Kawelela ambaye inadaiwa jina lake liliondolewa na uongozi wa chuo kwa madai kuwa alifeli somo moja na badala yake nafasi hiyo ilichukuliwa na Slivester Joseph pia nafasi ya makamu wa Rais jina la Veronika Msagira liliondolewa kwa madai kuwa tangu alipojiunga na chuo hicho miaka miwili iliyopita alikuwa bado haja sajiliwa.

Hata hivyo wanachuo kadhaa walichukuliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa lengo la kuwahoji kufuatia vurugu hizo ambazo zilizo sababisha mmoja ya viongozi wa chuo hicho kunusurika kipigo baada ya askari polisi kufika katika eneo la chuoni hapo.
Kwa upande wake kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa baadhi ya wanachuo walihojiwa na kuruhusiwa na kurudi chuoni kwao na jarada la uchunguzi kuhusiana na tukio hilo limefunguliwa.

Jitihada za waandishi wa habari zilifanywa za kuutafuta uongozi wa chuo lakini zilishindikana baada ya kutokupatikana ambapo baadaye mmoja wa viongozi wa chuo hicho aliyetambulika kwa jina la Dr Katayi aliongea kwa njia ya simu kuwa uchaguzi wa serikali ya wanachuo umesitishwa kwa kuwa baadhi ya wagombea hawakutimiza vigezo na siyo vinginevyo.

  MWISHO.

Chapisha Maoni

 
Top