0
MIONGONI MWA WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI GEOFREY NILAI
NA STEPHANO MANGO,SONGEA

WAJUMBE wanne wa kamati ya utendaji wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma(RPC) wamejiudhuru nafasi zao kutokana na mwenendo mbaya wa uongozi ukiwemo ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za chama na matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi wakubwa wa chama hicho


Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa hotel ya OK mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji waliojiudhuru Geofrey Nilai aliwataja wajumbe wenzake kuwa ni Kassian Nyandindi, Joseph Mwambije na Mpenda Mvula na kusema kuwa  kwa umoja wao wamejiudhuru nafasi zao ndani ya chama kuanzia machi mosi mwaka huu na watabaki kuwa wanachama wa kawaida

Nilai alisema kuwa wameamua kujiudhuru nafasi zao kwa manufaa ya chama ambapo alitaja mambo yaliowafanya wafikie hatua ya kujiudhuru ni pamoja na kutofanyika kwa vikao vya kamati ya utendaji kulingana na katiba ya chama,kutotolewa taarifa za fedha za chama kwa kipindi cha miaka mitatu na toka ufanyike kwa uchaguzi mkuu wa chama mwaka jana hakuna kikao kilichofanyika cha kukabidhiana mali za chama

Alisema kuwa sababu nyingine ni mwenyekiti wa chama hicho Andrew Kuchonjoma kushindwa kuitisha kikao cha kubadilisha watia sahihi kwenye akaunti za chama zilizopo benki na badala yake anatumiwa mwanachama wa kawaida ambaye sio kiongozi jambo ambalo ni kinyume na katiba ya chama na ushirikishwaji mdogo wa masuala ya chama kwa wajumbe wa kamati ya utendaji,pia kamati ya utendaji kutokabidhiwa vifaa vinavyotolewa na muungano wa klabu za waandishi wa habari nchini(UTPC)

Alieleza zaidi kuwa sababu nyingine ambayo imewafanya wajiudhuru ni kutoshirikishwa mradi wa redio ya chama licha ya kuwa kuna tetesi ya manunuzi ya vifaa vya redio hiyo lakini wajumbe wa kamati ya utendaji mpaka tunafikia uamuzi wa kujiudhuru mwenyekiti Kuchonjoma ameshindwa kuwaonyesha na kueleza thamani ya vifaa hivyo na kikao kilichomwagiza kwenda kuvinunua

Alisema kuwa sababu nyingine ni kufunguliwa kwa akaunti benki kwa ajiri ya maafa kwa waandishi wanachama wa RPC bila kuwashirikisha wanachama wenyewe pamoja na kamati ya utendaji, pia ilichangishwa michango kwa wadau mbalimbali kwa ajiri ya mradi wa redio lakini hakuna taarifa ya fedha iliyotolewa kwenye kamati ya utendaji juu ya fedha hizo

Alisema kuwa kutokana na sababu hizo kwa umoja wetu tumefikia uamuzi wa kutokuwa na imani na viongozi wakuu wa chama hicho na kwa hiali yetu tumeamua kujiudhuru nafasi hizo ili wanachama wapate fursa ya kuitisha uchaguzi mkuu mpya ili kuweza kupata viongozi bora ambao watafuata katiba ya chama na misingi ya utawala bora na tayari barua ya kujiudhuru tumeuandikia uongozi wa chama hicho na nakala ya barua hizo zimepelekwa muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania(UTPC) na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa taarifa za jambo hilo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma Andrew Kuchonjoma alipoulizwa kuhusiana na wajumbe wa kamati ya utendaji kujiudhuru, alikiri kupokea barua kutoka kwa wajumbe wake wa kamati ya utendaji ambao wamejiudhuru nafasi zao ndani ya chama
 

Kuchonjoma alisema kuwa kwa kuwa wao wameamua kuchukua maamuzi magumu ya kujiudhuru nyadhifa zao kwa hivi sasa wajumbe waliobakia kwa maana ya mwenyekiti, makamu mwenyekiti, mweka hazina na mweka hazina msaidizi wanaandaa mkutano maalumu wa uchaguzi wa kujaza nafasi za wajumbe waliojiudhuru
MWISHO

Chapisha Maoni

 
Top