AFISA MTENDAJI NA MWENZAKE WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUIDANGANYA TAKUKURU
KAMANDA WA TAKUKURU RUVUMA YUSTINA CHAGAKA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
TAASISI ya kuzuia na Kupamba na rushwa(TAKUKURU)Mkoani Ruvuma imewakamata watu wawili akiwemo Afisa Mtendaji wa kata ya Matogoro manipsaa ya Songea Peter Adam Mapunda na imewafungulia mashitaka ya kupokea rushwa na kusema uwongo mahakamani.
Akizungumza na Nipashe ijumaa iliyopita ofisini kwake kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupamba na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Ruvuma Yustina Chagaka alimtaja mshitakiwa mwingine kuwa Shaibu Ngonyani mkazi wa maeneo ya matogoro manispa ya songea.
Alifafanua zaidi kuwa kesi ya kwanza ni kesi ya jinai namba 45 ya mwaka 2016 ya jamhuri dhidi ya Shaibu Ngonyani ambaye alikuwa shahidi katika kesi ya jinai namba 38 ya mwaka 2015 ambayo ilikuwa imefunguliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani humo dhidi ya aliyekuwa Meya wa halmashauri ya manispaa ya songea amabaye pia alikuwa diwani wa kata ya matogoro kwa kosa la kutoa rusha kwa mshitakiwa Ngonyani ambaye wakati alitakiwa kutoa ushahidi mahakamani na baadaye aligeuka na kusema kuwa hakupewa rushwa ya aina yoyote na Mhagama jambo ambalo lilionekana kuwa ni tofauti na maelezo aliyokuwa ameyatoa kwa maafisa wa Takukuru wakati wakifanya uchunguzi wa malalamiko hayo.
Alisema awali mnamo agosti mwaka 2014 Takukuru Ruvuma ilipokea malalamiko toka kwa baadhi ya wananchi wa kata ya matogoro manispaa ya songea wakimtuhumu aliyekuwa diwani wa kata hiyo ambaye pia alikuwa Meya wa manispaa ya songea kuwa amejenga nyumba yake binafisi kwenye kiwanja cha ofisi ya serikali ya kata ya matogoro kiwanja ambacho walikuwa wameuziwa na Ngonyani
Alisema kuwa wakati Takukuru ikiendelea na uchunguzi wa malalamiko hayoNgonyani alihojiwa kuhusu eneo hilo ambapo alieleza kuwa eneo hilo alikuwa ameliuza kwa serikali ya kata ya matogoro na sio kwa mtu mwingine yoyote
Alieleza zaidi kuwa inadaiwa wananchi wa kata ya matogoro walipoanza kuhoji kwanini mhagama ameamua kujenga nyumba kwenye eneo la serikali hivyo mhagama alimfuata ngonyani na kumshawishi amwandikie hati ya maudhiano ya eneo hilo na kumpa fedha tasilimu ya shilingi (250,000) lakini Ngonyani alipoitwa mahakamani kutoa ushahidi wa kesi iliyokuwa inamkabili mhagama alikataa katakata kuwa hakupokea fedha ya aina yoyote toka kwa mhagama jambo ambalo mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa Ruvuma iliamua kumwachia mshtakiwa kwa madai kuwa ushahidi uliotolewa mahakamani hakuwa unaonyesha kuwa mhagama alitenda makosa hayo kisha kesi hiyo ilitupiliwa mbali.
Kesi ya Pili ni kesi ya jinai namba 46 ya mwaka 2016 ya jamhuri dhidi ya Afisa mtendaji wa kata ya Matogoro Mapunda ambaye alikuwa anatuhuma za kusema uwongo kinyume na kifungu cha 102 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya kanuni za adhabu ambapo Mapunda alikuwa ni shahidi wa Jamhuri katika kesi namba 38 ya mwaka 2015 ya jamhuri dhidi ya Charles mhagama amabye kwa wakati huo alikuwa diwani wa kata ya matogoro pia Meya wa halmashauri hiyo.
Alisema kuwa washitakiwa wote wawili wamekana mashitaka na wako nje kwa dhamana hadi itakapotajwa tena Aprili mwaka huu na kwamba kutokana na maelezo yao ya uwongo ilisababisa mshitakiwa mhagama kuonekana hana kosa la kujibu.
Amewaomba wananchi kuona umuhimu wa kutoa ushirikiano katika kufichua maovu na vitendo vya rushwa kkwa ustawi wa taifa letu la Tanzania na kwamba kwa watu wenye tabia mbaya wa kutoa ushahidi wa uwongo mahakamani hawata vumiliwa bado watachukuliwa hatua za kisheria kwani kutoa ushidi wa uwongo ni kosa la jinai na si vinginevyo.
MWISHO
Chapisha Maoni