0
Kwirinus Mapunda- Songea.
MKURUGENZI wa Hospitali ya Peramiho Dr. Ansgar Stuff (OSB) mewataka vijana kuinua vipaji vyao katika michezo ili taifa liweze kupata wanamichezo bora kama nchi nyingine zilizoendelea 
 
Hayo aliyasema mratiba wa mashindano Sixbert Komba kwa niaba ya Dr Asgar Stuff ambaye anafadhili michezo ya pasaka maarufu kwa jina la mashindano ya pasaka yanayofanyika Peramiho Songea vijijini
 
Komba alisema michezo hiyo ya mpira wa miguu na pete yanajumuisha kata sita, Maposeni peramiho Liganga, Mpandangindo, Litisha, Kilagano, Parangu madhumuni ya mashindano hayo ni kuinua  vipaji vya wanamichezo wa mpira wa miguu na pete (netball).
 
Aidha mratibu huyo wa michezo hiyo Sixbert Komba alisema mashindano hayo pia yana lengo la kuwaunganisha vijana kimwili na kiroho na kuondokana na fikra potofu zenye madhara kimaisha na kuongeza kipato kwa wananchi kwa kutoa fursa ya kufanyika biashara ndogondogo 
 
Aidha alisema mfadhili wa mashindano hayo atatoa zawadi kwa mshindi wa kwanza laki tano na mshindi wa pili laki nne pia mshindi wa tatu laki tatu na mchezaji bora Tsh Hamsini elfu katika ufunguzi wa michezo hiyo inayofanyika katika uwanja wa Asgar Peramiho Songea vijijini 
 
Alisema kuwa katika ufunguzi Parangu ilimenyana na Mpandangindo, matokeo Parangu walichabangwa mabao 2 kwa sifuri, wafungaji ni Samuel Luambano Dk, 56 na Kandidus Lugongo Dk, 83 
 
Alisema kuwa waamuzi walikuwa Kabanga Tambwe waamuzi wasaidizi Kananani Kasuga na Hamisi Mapunda, aidha mgeni rasmi alikuwa Tanu Kameka kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Songea. Mashindano yanaendelea kila jumamosi na jumapili
MWISHO
 

Chapisha Maoni

 
Top