Emmanuel Mlaponi akiwa na mama yake mzazi
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MTOTO Emmanuel Mlaponi (16) akiwa na wadogo zake wane na
mama yake wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuri
kuona umuhimu wa kuingilia kati sakata la kupatikana kwa mirathi ya baba yake
aliyepotea tangu mwaka 2005
Akizungumza na gazeti hili jana Emmanuel Mlaponi ambaye yupo
kidato cha pili alisema kuwa yeye na mama yake wamekuwa wakiishi maisha ya
taabu sana toka baba yake ambaye alikuwa anafanya kazi katika Hospital ya Rufaa
ya Mkoa wa Ruvuma alipopotea mwaka 2005
Kijana huyo anasema kuwa yeye na mama yake walipoona kuwa
Benedict Mlaponi amekata mawasiliano na ameshindwa kurudi walijitahidi kwenda
ofisini kwake kumuulizia bila mafanikio yoyote huku miaka inaenda ndipo
walipofungua mirathi yam zee huyo ili waweze kunufaika na jasho lake
Alisema kuwa mirathi ilifunguliwa na Serikali iliridhia tupewe
haki ya mzee wetu lakini mpaka sasa
hatujapata na hatujui kama ilichukuliwa au ndiyo majipu yanayo tumia fedha za
wajane na ndio maana sasa tunatapatapa ili tuweze kulipwa stahiki yetu
Naye mke wa Benedict Mlaponi aliyejitambulisha kwa jina
Angetruda Millinga akisimulia mkasa huo anasema kuwa mume wake alikuwa mfanyakazi
wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Songea na kwamba alipotea toka 13/10 /2005
mpaka leo hajulikani alipo.
Millinga anasema kuwa mara ya mwisho mume wake aliaga kuwa
anasafiri kikazi kwenda jijini Dar es salaam na alipata ruhusa kutoka kwa mkuu
wake wa kazi wakati huo alikuwa Dkt Wella hivyo toka wakati huo mpaka leo 2016
hajapatikana na haijulikani kama yuko hai au amekufa na kuwaacha watoto wake
watano pamoja na mimi ambaye ni mke wake wa ndoa
Mama huyo anasema mkuu wake wa kazi alipoona mtumishi wake
hayupo kazini kwa zaidi ya miezi 6 bila taarifa yoyote na bila kujua tatizo
lilompata masikini wa Mungu Benedict Mlaponi aliandikiwa barua ya
kufukuzwa kazini
“Mimi na familia tukashauliana namna ya
kufanya ndipo tukapitisha pombe ya mila na kuhesabu kuwa mume wangu amekufa na
tukaenda kutoa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi kilichopo Songea na tufungua
kesi ya mirathi”alisema Millinga
Alisema baada ya kutoa ripoti polisi na
kuona hapatikani Mahakama ikaamuru mimi na familia ya watoto watano tulipwe
fedha ya mirathi lakini Serikali ya Mkoa wa Ruvuma haijaweza kufanya hivyo hadi
sasa.
Alisema anawaomba wanaharakati
mbalimbali waweze kumsaidia kupata mirathi hiyo kwani amekuwa akiteseka sana
kuwalea watoto hao pekee yake toka mwaka 2005 hadi leo kwani naanza kukata tama
ya kupata haki ya mume wangu
Mume wangu alikuwa akifanya kazi Serikalini kwa nini
asilipwe mafao ya mirathi wakati kesi ilishapitia na kuthibitika kuwa mume
wangu kafariki katika mazingira ya kutatanisha ,hivyo namuomba Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt Magufuli anisaidie kwani nimeshakuwa mjane na
familia inanitegemea na hajulikani fedha
imeingia mikononi mwa majipu
MWISHO
Chapisha Maoni