0

NA STEPHANO MANGO,NAMTUMBO

WILAYA ya Namtumbo mkoani Ruvuma imejiwekea mikakati ya utengenezaji na ukarabati wa madawati kwenye shule za msingi na sekondari ambapo mahitaji ni 16,415 wakati yaliyopo kwa sasa ni 10,871 na upungufu kwa sasa ni 1,380.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo  Alqueen Ndimbo wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo kwenye baraza la madiwani la halmashauri ya namtumbo.

Alisema kuwa wananchi wanapaswa kuhimizwa juu ya utengenezaji na ukarabati wa madawati kwani wilaya ya Namtumbo inamaeneo mengi yenye misitu ya asili hivyo ni rahisi zaidi  kukamiliza zoezi hilo ilimradi tu sheria zifuatwe.

Alieleza kuwa kuwa zipo chanagamoto zinazojitokeza ambazo tayari zimeshaanza kufanyiwa kazi kwa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na madawati ya kutosheleza idadi ya wanafunzi waliopo kwenye shule za msingi na sekondari na si vinginevyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Daniel Nyambo alisema kuwa ili kuendana na kazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

Watumishi wa Halmashauri hiyo wametaakiwa kufanya kazi kwa uhadilifu na waepukane na tamaa ya kujitafutia fedha kwa njia za mikato na kuweza  kuisababishia hasara halmashauri hiyo.

Alisema kuwa kwa mfanyakazi yeyote atakayeona anabanwa sehemu yake ya kazi ajiondoe yeye mwenyewe aende akatafute mahali ambapo anaona ni rahisi kufanya mambo yake ambayo ni kinyume na taratibu na kanuni za kazi.

alifafanua zaidi kuwa katika zoezi la kuhakiki watumishi hewa mpaka juzi halmashauri ya wilaya ya Namtumbo imebaini kuwa kuwepo kwa watumishi hewa watano na bado kazi ya kuhakiki watumishi hewa inaendelea.

Naye mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Ally Mpenye alisema kuwa halmashauri yake imepanga kukusanya jumla ya shilingi 25,763,592,400.00 kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo mamlaka ya maji safi na maji taka, Leseni, Ruzuku toka serikali kuu, Wahisani, michango mingine pamoja mpango wa maendeleo.

Aliwataka madiwani kuona umuhimu wa kuwahimiza watendaji wa vijiji na Kata kuhakikisha wanakusanya mapato kwenye maeneo yao kwa asilimia 80% na si vinginevyo.

MWISHO
 

Chapisha Maoni

 
Top