.
NA STEPHANO MANGO,NAMTUMBO
WANANCHI wa kijiji
cha Njalamatata kata ya mkongo
wilayani Namtumbo mkoani
Ruvuma wameaswa kuacha kuendeleza mgogoro wa eneo ambalo tayari
limemilikishwa kisheria na wamiliki wa eneo hilo walishakamilisha utaratibu wa
kisheria na walishapata kibali cha kumiliki eneo hilo.
Aidha afisa habari wa wilaya ya Namtumbo Yeremias Ngerangera alisema kuwa afisa ardhi wa wilaya ya Namtumbo bwana Maurus Hyera aliwaasa wananchi kuacha kuendeleza mgogoro
wa ardhi kati ya wananchi wa
kijiji cha Njalamatata na wamisionari wa Ligano jimbo la Songea kwa Madai ya wamisionari hao kumiliki eneo hilo kisheria.
Kwa mujibu wa afisa habari huyo madai ya wananchi hao
hayawezi kusikilizwa kwa sasa badala yake waiombe
halmashauri kupimiwa maeneo mengine iliwaendelee kufanya shuguli zao
za kilimo badala ya kulazimisha eneo ambalo linamilikiwa kisheria.
Hata hivyo bwana Ngerangera alitaja baadhi ya taratibu ambazo wamisionari
hao walizitekeleza ni pamoja na
kuomba ardhi hiyo katika kata ya mkongo
ambapo kijiji cha Njalamatata,mkongo na Nakawale
kiliridhia kuwapa ardhi
hiyo katika kikao chao cha tarehe 23.Desemba 1983.
Maamuzi hayo yalipelekwa kwenye kikao cha pamoja
cha kamati ndogo ya huduma ya
uchumi wilaya ya songea wakati huo ,
viongozi wa tarafa ya undendeule na
mkongo pamoja na uongozi
wa wamisionari hao katika kikao kilichofanyika 5mei 1987 na kufikia
uamuzi wa kuwapimia wamisionari hao eneo waliloomba kwa
madai kuwa uwepo
wa wamisionari hao utakuwa
na manufaa makubwa
kwa wananchi na kuvitaka vijiji hivyo kuonesha
ushirikiano katika kuheshimu
mipaka hiyo.
Pamoja na
hali hiyo mkulima wa kijiji
cha njalamatata bwana Selemani
ngonyani alisema kuwa kwa
sasa wanapata adha kubwa
ya kutafuta maeneo ya
kulima kwa kuwa
maeneo tegemewa yanamilikiwa
na wamisionari hao ,maeneo ambayo
yangeweza kuwainua kiuchumi kwa wananchi wa kijiji cha Njalamatata.
Wamisionari wa jimbo
la Songea waliomba Hekta 2500kutoka
katika vijiji hivyo na baada ya kupimiwa
zikapatikana Hekta 2007 sawa
na ekari 4947 ukiondoa sehemu
za mabonde walibakiwa
na Hekta 2002 .
Maeneo
yaliyoombwa yalikuwa kwa
matumizi ya ibada,elimu,huduma za
jamii,kujenga viwanda pamoja
na kuanzisha kilimo na
ufugaji ambapo eneo hilo lilisajiliwa na kupewa
hati ya shamba Na.39 ya tarehe 19machi1986.
Mwisho
Chapisha Maoni