WATATU MBARONI KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI NA BANGI
JESHI la Polisi Mkoa wa Ruvuma linawashikilia watu watatu wakazi wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma kwa kukutwa na nyara za serikali zikiwemo silaha,meno ya ngiri vipande 8 pamoja na bangi kilo 3.32
Akielezea tuhuma hizo Kamanda wa Oilisi wa Mkoa wa Ruvuma Zuber Mwombeji alisema kuwa mtuhumiwa Mustafa Yasini (42) mmatengo na mkazi wa Namtumbo alikamatwa akiwa na silaha aina ya shortgun greener,risasi 6,maganda 3 ya risasi,jino 1 la ngiri,vipande 5 vya maganda ya kakakuona,buti za jeshi jozi 1 na clown 1 ya jeshi la Polisi huko katika kijiji cha Namanina wilayani Namtumbo
Mwombeji aliwataja watuhumiwa wengine ni Juma Mapunda (42) mnindi mkazi wa Namtumbo na Kasimu Nchimbi (57) mmatengo mkazi wa Namtumbo walikamatwa wakiwa na bangi kilo 3.32,vipande 7 vya mano ya ngiri,baruti chupa 2 na goroli 56 za risasi huko katika kijiji cha Namali wilayani Namtumbo
Alisema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuwatafuta wahalifu wote na kuwafikisha mahakamani ili kuweza kupisha sheria kuchukua mkondo wake mara baada ya upelelezi kukamilika na kuwataka wananchi wenye mapenzi mema na nchi yao kutoa taarifa ya vitendo vyote viovu kwa mustakabali wa amani ya nchi yetu
“Ili kuhakikisha kwamba mkoa wetu unaendelea kuwa salama tunaendelea kuimarisha doria,misako na operesheni katika maeneo mbalimbali ili kufanikisha kuwakama waharifu wote ambao wanavuruga amani na utulivu miongoni mwa jamii”alisema Rpc Mwombeji
MWISHO
Chapisha Maoni