WATU 11 MBARONI KWA KUKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA NA GONGO RUVUMA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WATU 9 wamejikuta wakishikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kukutwa katika maeneo mbalimbali wakifanya biashara ya dawa za kulevya aina ya bangi kilo 96 na kete zake 176 na wengine wawili wamekamatwa wakiwa na pombe haramu ya moshi aina ya gongo lita 67
Akizungumza na gazeti hili Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuber Mwombeji aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Gabriel Ndabaliuze(37) mkulima na Mkazi wa Bombambili,Evance Mkonde(24) mkulima na Mkazi wa Lizaboni na Gwaita Shaib (35) mkulima na mkazi wa Namanditi wote kwa pamoja walikamatwa na bangi kilo 34 maeneo ya Matarawe Songea Mjini
Mwombeji alisema kuwa watuhumiwa Costa Mwinuka (49) mkulima na mngoni mkazi wa Mkuzo,Angeleus Hyera (39) mmatengo mkulima mkazi wa Lupapila,Zamtanga Gama (42)nngoni na ni dereva mkazi wa Mjimwema walikutwa eneo la sido Songea wakiwa na bangi kilo 41
Aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Felician Mgaya (44)mbena,Mustapha Rashid,Mrisho Mponda(19) mkazi wa Hoahoa Mbinga walikamatwa na bangi kilo 7 na kete 132 na Hija Omari Hashimu wa Nakapanya Tunduru alikamatwa na bangi kilo 5
Kamanda huyo alimtaja Hasani Mtulule (32) myao na Twalib Abas (30) mmakua mkazi wa Tunduru walikamatwa na pombe haramu ya moshi ya gongo lita 67 na kwamba upelelezi unaendelea na mara utakapo kamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili
MWISHO
Chapisha Maoni