0

Pamoja na kwamba nimefurahi kuona hatua kali za kisheria zimeanza kuchukuliwa dhidi ya makatili wauaji wa Albino lakini kwa jinsi ninavyoumizwa na vitendo hivyo bado ninaona adhabu ya kifo kwa watu hao ni nyepesi na ni kuwapendelea.

Adhabu hiyo haitoi nafasi kwa katili husika kujutia matendo aliyoyafanya wala haitoi nafasi nzuri kwa watu wengine kujifunza kutoka kwa mtu huyo. 

Ukinipa nafasi ya kupendekeza adhaba .. na nadhani nipendekeze adhabu mbadala kwa makatili hawa .. Ni vema sasa Serikali ikatunga sheria zitakazoruhusu adhabu zifuatazo.. 

Mtu atakayethibitika kufanya ukatili kwa Albino au hata wauaji wa vikongwe basi ahukumiwe kukatwa viungo na yeye kama alivyomfanyia mtu aliyemfanyia ukatili, na adhabu hiyo itekelezwe bila ganzi kama wao walivyofanya .. lakini kabla ya utekelezaje wa adhabu hiyo .. 

mtu husika chini ya ulinzi mkali apelekwe eneo alilotekeleza unyama wake na katika mkutaano wa hadhara atandikwe viboko 50 ..

 kisha chini ya ulinzi mkali apelekwe anakoishi mbele ya mkutano wa hadhara ndugu jama na rafiki zake washuhudia atandikwe tena viboko 50 kisha apelekwe kwa watekelezaji wa adhabu ya kuondoa viungo vyake .. 

kisha atibiwe na aendelee na maisha yake ili nao wakae wakitesema maisha yao yote kama hao waliowafanyia ukatili wakasalimika wanavyoteseka. Mpango huu utasaidia kuwapa wauaji nafasi ya kujiutia maisha yao yote na pia utawapa nafasi wengine kujifunza

Chapisha Maoni

 
Top