MWANASHERIA WA SONGEA KIZIMBANI KWA RUSHWA
NA,STEPHANO MANGO,SONGEA
MWANASHERIA wa Halmashauri ya Wilaya Songea Hotay Tluway (43) Na Slavian Mbarare mkazi wa kijiji cha Makwaya kata ya Muhukuru wilayani songea wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi mkoani Ruvuma kujibu mashtaka mawili ya kutoa rushwa ya shilingi 330,000 elfu kwa hakimu wa mahakama ya wilaya ya songea kwa lengo la kumshawishi ili aangalie uwezekano wa kuifuta kesi ya mali asili inayowakabili baadhi ya wanakijiji akiwemo mshatakiwa Mbarare.
Wakiwasomea mashtaka wastakiwa hao wanasheria wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ( TAKUKURU) Mkoani Ruvuma Gregory Joseph na Herman Malima walidai mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Ruvuma Simoni Kobelo kuwa washtakiwa wote wawili wanashtakiwa kwa makosa mawili.
Wanasheria hao walieleza kuwa kosa la kwanza ni la kukamatwa na rushwa kinyume na kifungu cha 15 kidogo cha kwanza “B” cha sheria ya uzuiaji na kupambana na rushwa namba 11 cha 2007 ambapo inadaiwa marchi 3 mwaka huu katika eneo la manaispaa ya songea kama mwanasheria wa halmashauri ya wilaya Tluway na mwenzake ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mkwaya Mbarare bila halali waliahidi kiasi cha fedha isieye julikana kwa kukuita maji ya kunywa kwa hakimu wa mahakama ya wilaya ambaye jina lake limehifadhiwa kumshawishi aweze kutoa hukumu ya upendeleo ambayo ingeweza kumsaidia mshtakiwa Mbarare kwa shitaka linalomkabili yeye pamoja na baadhi ya wanakijiji wenzake ambalo linahusiana na masuala ya mali ya asili.
Walisema kuwa Tluway na Mbarare pia wanashtakiwa kuwa mnamo march 3 mwaka huu kuwa mwanasheria pamoja na mwenzake pasipo halali walimpatia kiasi cha fedha shilingi 330,000 hakimu wa mahama ya wilaya ambaye jina lake limehifadhiwa kama kishawishi kwa lengo la kutaka aweze kutoa hukumu ambayo itamsaaidia mshtakiwa Mbarare kwa shauri ambalo lipo mbele yake ambalo linawahusisha na baadhi ya wanakijiji wenzake la mali asili.
Hata hivyo washtakiwa wote wawili wamekana mashtaka yao na kesi imeharishwa hadi march 19 mwaka huu itakapo tajwa tena na wastakiwa wote wawili wapo nje kwa dhamna ya shilingi milioni tatu kila mmoja.
MWISHO.
Chapisha Maoni