0
                           MEYA WA MANISPAA YA SONGEA CHARLES MHAGAMA


NA STEPHANO MANGO,SONGEA

MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Charles Mhagama (50) amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa Wilaya ya Songea akishitakiwa kwa kosa la rushwa kinyume na kifungu namba 15 kidogo 1B cha sheria ya uzuiaji na upambanaji wa rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Awali akisomewa shtaka hilo mbele ya hakimu mfawidi wa mahakama ya Wilaya ya Songea Elizabeth Missana mwendesha mashitaka toka TAKUKURU mkoani Ruvuma Greigory Joseph alisema kuwa manamo mwaka 2010 huko katika kata ya Matogoro Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma akiwa kama Diwani wa kata hiyo alimpaa Shaib Ngonyani SH.250,000 kama kishawishi cha kumwandikia mkataba feki wa mauziano ya kiwanja ambapo ni mali ya ofisi ya mtendaji wa kata ya Matogoro.

Hata hivyo mwanasheria wa TAKUKURU Joseph aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo ya jinai namba 38 ya mwaka 2015 imekamilika na wapo tayari kuendelea na shauri hilo na wako kwa kusikilizwa.

Hata mshitakiwa amekana shitaka linalomkabili na yupo nje kwa dhamana ya maneno ya sh. 250,000 na kesi hiyo itaaanza kusikilizwa hija za awali Aprili 16 mwaka huu.

MWISHO.



Chapisha Maoni

 
Top