NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WACHIMBAJI wadogo wadogo nchini wametakiwa kujitokeza kwa
wingi kujaza maombi ya kuchukua ruzuku kwa ajiri ya kuendeleza shughuli zao ili
ziweze kuwakomboa kiuchumi na kuipatia kipato serikali kutokana na uchimbaji
wao wa kisasa
Akizungumza jana na Waandishi wa habari ofisini kwake Kamishina
Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Nyasa
Fredy Mahobe alisema kuwa awamu
ya pili ya utolewaji wa ruzuku ulitangazwa rasmi februari 2 na mwisho
wa kupokea maombi ya ruzuku hizo ni machi 27 mwaka
Mahobe alisema kuwa kabla ya mwezi mei mwaka huu ruzuku
zinatakiwa ziwe zimetolewa kwa waliofanikiwa kushinda maandiko yao ya mradi ili
waweze kuongeza mitaji yao katika kufanikisha shughuli husika
Alisema kuwa Serikali kupitia Benki ya Dunia toka mwaka 2013
iliamua kuwaendeleza wachimbaji wadogo kwa kuwapa ruzuku katika mradi wake
kuendeleza sekta ya madini nchini ili waweze kujikomboa na kuiongezea kipato
serikali kutokana na kodi watakazokuwa wanazilipa katika biashara ya madini
nchini
Alieleza kuwa kwa mwaka huu wa fedha 2015/2016 benki ya
dunia imetoa dola laki moja kwa ajiri ya kuwaendeleza wachimbaji ili waweze
kuchimba kwa kutumia vifaa vya ili wajipatie vipato na kuingizia mapato
serikali
Alisema kuwa wachimbaji wanatakiwa kutembelea ofisi za
madini kwenye kanda au popote zilipo nchini ili waweze kupata maelekezo ya
kutosha namna ya kuwasilisha maombi ya miradi ya uchimbaji kabla ya msimu
kwisha ili waweze kunufaika na fedha hizo kutoka benki ya dunia
MWISHO
Chapisha Maoni