0
MFANYABIASHARA GOLDEN SANGA (SANGA ONE)

NA STEPHANO MANGO,SONGEA

BAADHI ya wakazi wa Manispaa ya Songea mkoa wa Ruvuma wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kwa kutafuta usuruhishi na wafaanya biashara ambao wamegoma kufungua biashara zao na kusababisha kuwepo kero kubwa kwa wananchi wakiwemo wanaishi vijinini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini Songea wakazi hao wameeleza kuwa kitendo cha wafanya biashara kufunga maduka, daladala na bodaboda wananchi wengi wameanza kupata usumbufu kwa kukosa mahitaji yao waliokuwa wamefuata kutoa vijijini wanakoishi.

Hebron Komba mkazi wa mwenge mshindo amesema  kuwa katika hali isiyo ya kawaida amelazimika kutembea kwa mguu kutoka mwenge mshindo kwenda songea mjini ambako alikuwa anataka kununua mbolea lakini alipofika katikati ya mji ghafla alishangaa kuona maduka yote yamefungwa jambo ambalo amedai kuwa ni kero kwako.

John Kumburu mkazi wa eneo la mtaa wa Likuyufusi kata ya Lilambo  alisema kuwa hatua waliyochukua kufunga maduka ni kubwa mno hivyo ameiomba serikali hichukue hatua za haraka kwa kukaa na wafanya biashara ili kulimaliza tatizo lililopo ambalo limesababisha wananchi wengi kukosa huduma za msingi.

Baadhi ya waandishi walishuhudia katika maeneo ya katikati ya manispaa ya Songea maduka yakiwa yamefungwa pamoja na eneo la sokuu ambako huduma zote zimesimama na watu wengi wakionekana wakitembea kwa miguu  baada ya daladala na bodaboda kugoma.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Jumuhiya ya wafanyabiashara Tanzania mkoani Ruvuma Isoma Mbilinyi alisema kuwa  wafanya biashara wamelazimika kufunga biashara zao ni baada ya kukubaliana kwenye mkutano mkuu wa jumuhiya hiyo  uliofanyika kwenye  ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki jimbo kuu la songea parokia ya Bombambili ambako  waliazimia kwa pamoja kwa lengo la kuishinikiza serikali isikilize kilio chao.

Ameiomba serikali kuona umuhimu wa kuchukua hatua kwa kuwasilikiza wafanya biashara ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilia juu ya ongezeko la kodi ya mapato  kwa asilimia 100% na tatizo la mashine za EFD.

Alifafanua zaidi kuwa  wafanya biashara kamwe hawakatai kulipa kodi ya serikali  lakini ombi lao kubwa ni kuona umuhimu wa serikali kupunguza kodi ya mapato ambayo imepandishwa kwa asilimia 100% na kwamba mwenye kiti wa jumuhiya hiyo ya Taifa ambaye yupo mahabusu Johson Minja mamlaka zinazohusika zione umuhimu wa kumuachia kwa dhamana.

Naye Golden Sanga amewahasa wafanya biashara wa songea kuwa na mshikamano wa pamoja kwa kufanya maamuzi ambayo yatasababisha  serikali iwaonee huruma kwa kusiliza kilio chao na amewataka wasiwe na jazba isyokuwa na msingi ambayoa haitaweza kuwaletea tija.

Afisa masoko wa halmashauri ya manispaa ya songea Salumu Homera alipohojiwa na Waandishi wa haabari ofisini kwake jana mchana alikiri kuwa  soko kuu la Songea wafanya biashara wamefunga maduka yao  jambo ambalo limeikosesha halmashauri  mapato na jitihada zinafanywa ili kuona namna ya kukaa na wafanya biashara hao waweze kufungua biashara zao.

Hata hivyo kaimu meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Ruvuma Lamson Tulyanje amewaambia kuwa ofisi yake haina taarifa yoyote kuhusu mgomo huo wa wafanya biashara lakini alidai kuwa kodi wamekuwa wakifika kulipa bia kuwepo matatizo ya aina yoyote.

MWISHO.




Chapisha Maoni

 
Top