0
MEYA WA MANISPAA YA SONGEA CHARLES MHAGAMA

NA,STEPHANO MANGO,SONGEA

MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Charles Mhagama (50) anayekabiliwa na shtaka la rushwa kinyume na kifungu cha  namba 15(1) B cha sheria ya uzuiaji na upambanaji wa rushwa namba 11 ya mwaka 2007 amepanda kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Songea kusomewa hoja za awali za shitaka linalomkabili.

Katika Mahakama hiyo iliyokuwa imefulika watu waliokuja kusikiliza kesi hiyo waendesha Mashtaka wawili wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)mkoani Ruvuma Chali Kadege na Helman Malima mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Elizabeth Missana walisoma hoja 14 za maelezo ya awali ambapo hoja ya kwanza mshitakiwa Charles Mhagama (50)ambaye ni Diwani wa kata ya Matogoro manispaa ya Songea.

Walisema kuwa hoja ya pili baadhi ya majukumu yake kama diwani mshitakiwa kama diwani ni kuwawakilisha wananchi wa kata yake katika baraza la madiwani la halmashauri ya manispaa hiyo na kwamujibu wa majukumu yake ya udiwani mshitakiwa Mhagama ni mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata.

Walieleza zaidi mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Mhagama alijenga nyumba pembeni ya ofisi ya kata ya matogoro katika eneo la kata hiyo ambapo ofisi mpya ya kata ilishajengwa na mwaka 2010 mshitakiwa Mhagama alimfuata Shaib Ngonyani na akamweleza kuwa yeye ndiye anayejenga nyumba kwenye eneo la ofisi ya kata ya Matogoro.

Walifafanuwa zaidi kuwa mwaka 2011 mshitakiwa alianza kujenga nyumba pembeni ya ofisi ya kata ya Matogoro na manamo mwezi wa 12 mwaka 2011 kuliitishwa mkutano na ofisi ya kata ya Matogoro na diwani huyo alikuwepo na alipewa malalamiko ya ujenzi wa nyumba kwenye eneo la ofisi ya kata.

Mawakili hao wasomi wa TAKUKURU waliendelea kutoa hoja za awali mahakamani hapo kuwa mwaka 2011 wananchi wenye hasira walibomoa nyumba aliyokuwa anajenga nyumba na baadae alienda kushitaki polisi ambapo polisi wakishilikiana na yeye walikwenda kuwakamata Mohamed Mvula na Seif Abdlah .

Walisoma hoja nyingine kuwa mshitakiwa alimuomba Shaibi ngonyani amuandikie hati ya mauziano ya eneo ambalo yeye alikuwa anajenga nyumba ambapo mwaka 2010 alimshawishi Shaibu Ngonyani kwa kumpa kiasi cha sh. 250,000/=ambayo aliitoa kwa nyakati tofauti mpaka ilipotimia.

Waliieleza mahakama kuwa mshitakiwa Mhagama alimwambia Ngonyani kuwa hela hiyo ni ya chai kwani nyumba ameshajenga hivyo hakuna mtu yeyote atakaye mshitaki ,wakati anajenga nyumba hiyo tayari ofisi ya kata ilikuwa imeshajengwa na hiyo kata Mhugama ndiye diwani na haliweza kumshawishi Ayubu Singwa awe shahidi wa siku ambayo ngonyani alimwandikia hati ya mauziano.

Hata hivyo mshitakiwa ambaye pia ni diwani wa kata ya Matogoro alikubaliana na hoja sita alizosomewa kati ya hoja 14 zilizosomwa mahakamani hapo ambapo aliongozwa na wakili anayemtetea wa kujitegemea Abel Ngilangwa na upande wa mashitaka ukiongozwa na mawakili wawili ulidai kuwa wanatarajia kuleta mashaidi 13 na vielelezo 4 na kwamba kesi hiyo imehairishwa hadi 15 mei mwaka huu.

MWISHO.

Chapisha Maoni

 
Top