NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WATUMIAJI wa Maji katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea
Mkoani Ruvuma wametakiwa kuyatumia maji hayo kwa uangalifu ili yaweze kuwafikia
na wengine wenye mahitaji muhimu kwa afya zao
Wito huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya
Maji Safi na Maji taka Wilaya ya Songea (SOUWASA) Mhandisi Wilson Mandia
alipokuwa anatembelea vyanzo mbalimbali vya maji vilivyopo Ruhila, Mahilo na
Matogoro mjini hapa
Mandia alisema kuwa Souwasa inatumia gharama nyingi sana
katika kuyahifadhi, kuyatibu na kumfikishia mlaji kwa gharama nafuu lakini
mtumiaji anayatumia maji hayo kwa fujo kana kwamba yanaendana na malipo yake
Alisema kuwa wapo watumiaji wengi wanatumia maji hayo
kumwagilia bustani mbalimbali za maua au mboga na wengine huoshea magari ,
pikipiki, bajaji na baiskeri wakati maji hayo yapo mahususi kwa ajiri ya
matumizi ya kunywa na kupikia na matumizi mengine madogomadogo ya majumbani
Alieleza kuwa vitendo hivyo vinaisababishia mamlaka hasara
kubwa kwani maji mengi yanatumika kwa matumizi ya ovyo na kusababisha watumiaji
wengine kukosa maji na pia kushindwa kuwasambazia wahitaji wengine ambao
hawajafikiwa na mtandao wa maji safi na salama
“Mamlaka ya Songea imepewa cheti cha kuwa na maji yenye
ubora kuliko mamlaka zingine Tanzania kutokana na namna maji yetu
tunavyoyahifadhi, yatibu na kuyasambaza kwa watumiaji hivyo ni vyema yakatumika
kwa malengo kusudiwa na sio vinginevyo” alisema Mandia
Naye Mkurugenzi wa Souwasa Mhandisi Francis Kapongo alisema
kuwa licha ya kuwasambazia wakazi wa Manispaa huduma ya Maji safi na Salama kwa
asilimia 75 tumekuwa tukipata changamoto nyingi sana katika kuendesha mamlaka
hiyo
Kapongo alisema kuwa watumiaji wengi wamekuwa wakichelewesha
kulipa ankra zao kwa wakati na kusababisha usumbufu mkubwa kwa uendeshaji wa mamlaka kutokana na kutokuwa na
vyanzo vingine vya mapato
MWISHO
Chapisha Maoni