NA STEPHANO MANGO, SONGEA
MWENYEKITI wa Chama cha Walimu, CWT
Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Mathias Mwanjisi ameutaka uongozi wa Manispaa
hiyo unaoshughulikia matatizo ya Walimu kuhakikisha wanawapandisha
madaraja Walimu wote wanaostahili ili kuondoa malalamiko kwa baadhi yao ,ambao
kwa muda mrefu hawajapandishwa licha ya kuwa na vigezo.
Mwanjisi aliyasema hayo jana wakati wa uchaguzi wa mkutano mkuu wa viongozi wa Chama hicho ambapo Mwenyekiti huyo alishinda kwa kura 84 huku mpinzani wake Edimundi Nditi alipata kura 18 huku idadi ya wapiga kura ilikuwa 102 na msimamizi wa uchaguzi ,Efigenia Nzota kutangaza matokea ya uchaguzi huo.
Kiongozi huyo aliyetetea nafasi yake awali kabla ya uchaguzi walipokuwa wakipitia utekelezaji wa chama hicho na mafanikio yake alisema kuwa changamoto kubwa ni kwa baadhi ya walimu ambao wanastahili kupandishwa madaraja kushindwa kufanyiwa hivyo kwa wakati na hatimaye kutengeneza malalamiko dhidi yao.
Alisema kuwa ili kuondoa dhana hiyo ya malalamiko ni lazima viongozi wa kitengo husika cha Manispaa kupeleka taarifa zote za walimu wanao stahili kupanda madaraja katika ofisi husika za makao makuu na kufanyiwa kazi kwa haraka.
Aidha mwenyekiti huyo akitoa neno la shukrani mara tu baada ya kuchaguliwa kwa wajumbe hao alisema kuwa kazi kubwa ni kushikamana kukijenga chama chao kwakuepusha migogoro ambayo inaweza kuwagawa bila sababu za msingi ambazo zitakigarimu chama.
“Naomba tushikamane kukijenga chama chetu kwa kuwa tusiposhikamana tutakiharibu chama na matokeo yake chama kitaingia kwenye migogoro ambayo inaweza ikagarimu jambo ambalo siyo jema mbele za jamii wanaotutegemea”alisema mwenyekiti wa CWT.
Hata hivyo katika uchaguzi huo nafasi mbalimbali ziligombewa ikiwemo ya uweka hazina ambapo ,Emmnuel Kayuza alipita bila kupingwa kutokana na mpinzani wake ,Ananias Mbilinyi kujitoa huku nafasi ya uwakilishi walimu wanawake aliibuka mshindi ,Sophia Luoga ambaye aliwabwaga wapinzani wake watano.
Kwa upande mwakilishi wa CWT mkoa wa Ruvuma ngazi ya Taifa Jema Mapunda aliwataka viongozi wapya waliochaguliwa kwa sasa wanapaswa kufanya kazi kwa biddi hasa wakitambua kuwa kazi kubwa waliyonayo ni kuwatumikia walimu kwa lengo la kuhakikisha kuwa kero zao zinashughulikiwa.
MWISHO.

Chapisha Maoni