0


JESHI  la Polisi Mkoani Ruvuma linawasaka watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majangiri ambao walitelekeza vipande 11 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya shilingi 133,800,000 kwenye basi  la abiria waliokuwa wakisafiria kutoka Tunduru kwenda Songea.
 

Akizungumza na mangokwetu.blogspot.com jana ofisini kwake Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Yahaya Athumani alisema kuwa tukio hilo limetokea juziu majira ya saa 10 jioni wakati watu wawili ambao wanasadikiwa kuwa ni majingiri  waliposhtukiwa na abiria  baada ya kubaini kuwa mizigo waliyokuwa wamebeba ilikuwa si ya kawaida.
 

Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio watu wawili ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja walipandia njiani kwenye basi la kampuni ya Alkarimu lenye namba za usajiri  T 559 BHA linalosafirisha abiria kutoka Tunduru kwenda Songea.
 

Kaimu kamanda Athumani alieleza zaidi kuwa mjangiri hao inadaiwa walipanda kwenye basi hilo wakiwa wamebeba mabegi mawili na walipofika katika kijiji cha kilimasela walianza kuwa na hofu kuwa baadhi ya abiria wamewashtukia  wakaanza kumuomba konda asimame ili wabadili usafiri lakini dereva wa Gari hiyo aliendelea na safari.

Alisema kuwa watu hao waliendelea kumuomba kondakta ili washuke kwa madai kuwa wanataka kutumia pikipiki za kukodi na mabegi yao wayaache kwenye basi ndipo abiria waliwahoji majangiri hao kuwa kwanini wasishuke na mabegi yao.


Alifafanua zaidi kuwa dereva wa gari hilo baada ya kuona kuwa kunamvutano mkubwa kati ya abiria na hao majangiri aliamua kusimamisha gari ndipo majangiri hayo yalishuka na kukimbilia polini kisha basi iliendelea na safari hadi Namtumbo mjini ambako abiria walitoa taarifa katika kituo kikuu cha polisi Namtumnbo ambapo askari polisi walilazimika kupekua mabegi hayo na kubaini  kuwa ndani yake kulikuwa na vipande 11 vya meno ya Tembo.


Alieleza kuwa baada ya kubaini nyara za serikali polisi iliwasiliana na maafisa wa idara ya wanyama pori ambao walifika na kupima uzito wa vipande` hivyo vya nyara za serikali ambao ulibainika kuwa kilogramu 13.76 na jeshi la polisi linaendelea kuwasaka watuhumiwa hao na wakipatikana watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yao.

MWISHO

Chapisha Maoni

 
Top