0
 Shamba la mkulima hasiyefuata kanuni za kilimo hifadhi yaani kilimo holela ambacho kinapelekea mmomonyoko wa udongo kwa urahisi, pia Kuhusiana na Umhimu wa Kilimo Hifadhi katika mabadiliko ya Tabia nchi Bw. Abiud Gamba alieleza kuwa Kilimo cha mazoea cha kukatua na kupindua udongo siyo endelevu na kinachangia katika uharibifu wa ardhi na mazingira na hivyo kuongeza athari za Tabianchi. Kilimo Hifadhi ni jibu la kupunguza athari za mabadiliko ya Tabia nchi na hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao na usalama wa chakula ikiwa tu tufuata kanuni kuu tatu ambazo ni:
1. Kutifua udongo kwa kiwango kidogo au kutotifua kabisa 2. Kufunika udongo muda wote; kutochoma uoto asili na masalia ya mazao baada ya mavuno 3. Kilimo cha mzunguko au mbadilishano wa mazao na ya jamii ya mikunde/mazao na mchanganyiko na miti zaiad mtaalam huyo alisema Kulima kwa kutifua udongo kwa kiwango kidogo au kutotifua kabisa kunaongeza uwezo wa ardhi kuhifadhi maji, kuingiza hewa, kurahisisha kutiririka maji, kupata joto na kuhifadhi hewa ukaa ndani ya udongo"

"

 Wakulima wakiwa na mavuno yao yaliyotokana na majaribio yaliyofanyika katika teknolojia mbalimbali. kuonyesha mavuno yanayoweza kupatikana kwa kufuata kanuni sahihi za kilimo hifadhi.
 Aliye vaa kofia ni mratibu wa shughuli za mradi na Afisa Ugani kutoka Taasisi ya ACTN Bw. Abiud Gamba
Shamba la kilimo Hifadhi likiwa limefunikwa na mazao funika jamii ya mikunde
 Mkulima Kiongozi wa shamba la majaribio ya Kilimo Hifadhi Bw. Wernery Nindi kutoka kijiji cha Namatuhi wilaya ya Songea Vijijini akiwa shambani kwake
Afisa Mradi  Bw. Deogratias Ngotio na Mtaalam kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Uyole wakieleza jinsi ya kuchukua sampuli za udongo kwa wakulima na aliye vaa kofia nyeusi ni Bi Rabbie Harawa Afisa na Mtaalam wa Sayansi/Afya ya udongo kutoka AGRA Nairobi

 Mkurugenzi wa Wilaya ya Namtumbo Bw. Ally Mpenye akihojiana na mkulima wa shamaba darasa Bw. Mabigili wakati wakati wa maadhimisho ya siku ya wakulima Namtumbo yaliandaliwa na Taasisi ya ACTN
 Mtaalam wa Kilimo Hifadhi kutoka ACTN akitoa maelezo ya kina juu ya teknolojia ya kilimo hifadhi na urutubishaji uhusishi wa udongo wakati wa siku ya wakulima iliyofanyika kijiji cha mchomoro


Chapisha Maoni

 
Top