REHEMA GWAYA AKIWA AMELAZWA HOSPITAL YA MKOA WA SONGEA BAADA YA KUJERUHIWA NA MKE MWANZAKE KWA KUMWAGIWA MAFUTA YA MOTO |
REHEMA GWAYA AKIWA ANAMNYONYESHA MTOTO WAKE HUKU AKIWA AMELAZWA KATIKA HOSPITAL YA MKOA WA SONGEA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WAANDISHI wa Habari nchini wametakiwa kuandika
habari za kuibua changamoto mbali mbali zinazowakabili wazee ikiwemo
kuishinikiza serikali kutunga sheria ya sera ya taifa ya wazee juu
ya ulipwaji wa pensheni kwa wazee wote, hukosefu wa huduma za afya pamoja
na ulemavu wa kimaumbile unaosababishwa na uzee.
Wito huo umetolewa jana
na Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali linalohudumia Wazee (PADI )
Iskaka Msigwa wakati wa Mdahalo ulioshirikisha Waandishi wa habari, Wazee
na wakuu wa Idara wa halmashauri zote mbili za Halmashauri ya Songea
uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa shirika hilo wa Unangwa
uliopo Manispaa ya Songea.
Alisema,bado wazee
wanachangamoto nyingi ambapo uchambuzi wa sera na matamko maalum juu ya
stahili za wazee imekua changamoto kwani bado hali za wazee ni
mbaya kutokana na kuwepo na matukio mengi ya mauji ya vikongwe kwa imani za
kishirikina na kuwepo kwa huduma mbovu za matatibabu.
“kitendo chaserikali ya
Tanzania kutayarisha sera,mikakati na miundo mbinu mbali mbali aya utekelezaji
kuhusiana na maswala ya wazee ni ishara kwamba inatambua umuhimu wa wazee kama
rasilimali na hazina muhimu kwa maendeleo ya taifa lakini imekuwa ndivyo sivyo
,”alisema Msigwa
Kwa upande wao wazee
walioshiriki mdhalo huo wamesema kuwa japokuwa wameitumikia serikali kwa miaka
mingi lakini michango yao imekua haitambuliki kwa serikali hivyo
ameomba kuona umuhimu wa kuwasaidia wazeee .
Mmoja wa Wazee hao Sophia
Hasara mkazi wa Majengo Manispaa ya Songea ,aliomba serikali kuwaingiza
wazee kwenye mfuko wa bima ya afya (NHIF)badala ya ilivyo sasa wanatibiwa
kwenye mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambao unamipaka na changamoto nyingi
ikiwemo ukosefu wa madawa, ukosefu wa madakitari maalumu kwa ajili ya wazee na
vyumba vya matibabu jambo linasababisha ongezeko la vifo vya wazee.
“Japo kuwa taifa
linaonyesha kutotutambuaa lakini karibu kila jambo gumu tunaachiwa wazee ,
mfano ikitokea msiba tunaoitwa kuosha maiti ni wazee, kulea watoto Yatima
jukumu ilo tumeachiwa wazee,migogoro ya ndoa , wagonjwa sugu pamoja na
wanasiasa wakitaka kugombea wanatuona wazee kwanini serikali inapata kigugumizi
kutupa pensheni Wazee,”alisema
Naye Mzee Daud Mpangala
,mkazzi wa Matalawe ambaye ni katibu wa baraza huru la wazee Manispaa
alisema, wazee wamekuwa serikali kwa kupitia kila halmashauri inatakiwa kutenga
bajeti kwai ya kuwatunza wazee kwa kutoa mikopo ya bei naafuu ili waweze kufuga
kuku,ng’ombe na kuanzisha kilimo cha bustani iliwaweze kujikwamua kimaisha
badala ya kuomba omba.
Mdahalo huo wa siku
mbili umeshirikisha waandishi wa habari , wazee wa Manispaa ya Songea na wazee
wa songea vijijini ,wakuu wa idara mbali mbali toka toka halmashauri
mbili za Songea na Manispaa.
Mwisho.
Chapisha Maoni