STEPHANO MANGO,SONGEA
JIMBO la Mbinga Magharibi wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma
linajumla ya kata 21 miongoni mwa kata hizo ni Kata ya Chiwanda yenye Vijiji
Vitano ambavyo ni Ng’ombo, Kwambe, Chimate, Chiwindi na Mtupale
Kata hiyo kama zilivyokata zingine Tanzania mwaka huu
ifikapo agosti 25 zinatafanya uchaguzi wa kuwapata madiwani wapya baada ya wale
ambao walichaguliwa mwaka 2010 kumaliza kipindi chao cha uwakilishi wa miaka
mitano kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Nimepata kuzungumza na Kada wa chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Mathayo Patrick Kaimaima na kuzungumza naye mambo machache
ambayo yamemfanya ajitokeze mbele ya wananchi na wanachama wenzake achukue fomu
ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na kupigiwa kura katika uchaguzi wa mwaka huu kwa nafasi ya
udiwani wa chadema
Kaimaima alisema katika vijiji vitano ambavyo vinazunguka
kata ya Chiwanda imebahatika kuwa na Shule za msingi kila kijiji ambazo zilijengwa
kwa nguvu za wananchi lakini hadi sasa mchango wa Serikali katika kuwapeleka
walimu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na nyumba za walimu
umekuwa mdogo sana hali ambayo imekuwa ikidumaza elimu
Alisema kuwa kuna Sekondari moja tu ambayo inaitwa Nyasa
ambayo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na vifaa muhimu kwa
ajiri ya kutolea elimu ikiwemo vya kufundishia na kujifunzia, miundombinu, yake
sio rafiki kwa wanafunzi kuweza kupokea elimu stahiki, hakuna maabara, mabweni
walimu wa masomo ya sayansi na hesabu wa kutosha na nyumba zao za kuishi ambazo
zinatakiwa ziwe jilani na shule, maji na vyoo hakuna na hata madawati
“Hata ufaulu wa wanafunzi toka darasa la saba kwenda kidato
cha kwanza ni mdogo sana na wengine ambao wanafahauru wamekuwa wakishindwa
kuripoti mashuleni kwao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ada, mimba,
kilimo, utoro na sababu nyinginezo ambazo wanakutana nazo kwenye kaya
zao”alisema Kaimaima
Katika Kata hiyo yenye vijiji hivyo vitano ni kijiji kimoja
tuu cha Ng’ombo ambacho kimebahatika kuwa na huduma ya maji safi na salama kwa
ajiri ya matumizi ya binadamu lakini katika vijiji vingine huduma hiyo haipo na
kuwafanya wananchi wake kupata huduma ya maji ambayo sio salama kutoka kwenye
mifereji iliyopo mabondeni au kwenye visima vilivyochimbwa karibu na makazi yao
yaliyozungukwa na vyoo hali ambayo inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa
Jambo jingine ambalo ni la muhimu sana ni suala la mazingira
ambalo kimsingi ni suala mtambuka ambapo kwenye kata ya Chiwanda kutokana na
siasa chafu zinazofanywa na Diwani wa Kata hiyo Oddo Mwisho kupitia chama cha
Mapinduzi kwa maslahi yake ameweza kushirikiana na wamatengo wa mbinga kuvamia
maeneo muhimu ya misistu na kukata miti ovyo hali ambayo imesababisha mazingira
kuathirika kutokana na shughuli za ukataji miti na ulimaji wa ovyo usiozingatia
kanuni bora za kilimo na uifadhi wa mazingira
Kwa suala la afya ambalo ndio nguzo kubwa ya maisha ya
binadamu yoyote yule duniani lakini
kwenye kata ya Chiwanda kuna Zahanati hizo kuna changamoto kubwa sana za
upatikanaji wa dawa, watumishi na hata miundombinu yake sio rafiki kwa wagonjwa
hali ambayo inapelekea wagonjwa na waganga kuishi kwa mashaka sana kutokana na
ukosefu wa matibabu stahiki na nyumba zao za kuishi waganga ambazo ziko mbali na Zahanati,
Ingawa pia zahanati ya kwambe imetengwa kabisa kwa sababu za
kisiasa na kufanya huduma zake kuwa mbaya na wananchi wake kwenda kutibiwa
kwenye zahanati nyingine, licha ya kuwa zahanati hiyo ilikusudiwa kupandishwa
hadhi kuwa kituo cha afya
Hila za diwani Oddo Mwisho ambaye pia ni mwenyeki wa Halmashauri
ya Wilaya ya Nyasa na Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Ruvuma ndizo zimesababisha
huduma za kiafya kuwa mbaya kwenye kata hiyo
Kata hiyo imebahatika kupata miradi ya kuiwezesha sekta ya
kilimo cha umwagiliaji ili ipige hatua na
kwamba kijiji cha Ng’ombo na kwambe lakini miradi hiyo imekumbwa na changamoto
kubwa ikiwemo ya uharibifu wa miundombinu ya maji, barabara na ukosefu wa
masoko ya mazao yatokanayo na miradi hiyo
Changamoto hizo zimesababisha kuwa na matumizi mabaya ya
fedha za umma ambazo zilitolewa na Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo
katika miradi hiyo na kuonekana kuwa
miradi hiyo imekuwa ya kisiasa zaidi kwa malengo ya wajanja wachache wasio na
nia njema ya maendeleo kwa kujichotea fedha kwa maslahi yao binafsi
Suala la miundombinu nalo limekuwa kero kubwa kwa wananchi
wa kata hiyo, kwani barabara ambayo inatoka makao makuu ya wilaya ya nyasa
ambayo ni mbambabay kuja kwenye kata
wakati wa kifuku haipitiki kutokana na
uchakavu wake na kusababisha wakina mama wajawazito kujifungulia
barabarani na wengine wafariki kutokana na miundombinu duni
Pia hata madaraja yake yametengenezwa chini ya kiwango
likiwemo daraja la Ruhekei eneo la Tembwe ambalo linatumiwa na wananchi wengi
kutoka kata ya chiwanda na mtipwili na kusababisha shuguli zao za kiuchumi na
kijamii kukwama wakati huo
Katika suala la uwazi na uwajibikaji kume kuwa na mambo
mengi katika miradi na michango ambayo wanatozwa wananchi au kuchangishwa na
fedha ambazo zinatolewa na serikali pamoja na wahisani taarifa zake za mapato
na matumizi zimekuwa hazisomwi kwenye mikutana ya hadhara lakini pia zimekuwa
haziwekwi kwenye mbao za matangazo
Hali hiyo imepelekea kuwa na giza nene kwenye miradi ya
maendeleo na kusababisha baadhi ya viongozi ambao sio waaminifu kufanya
ubadhirifu kwenye fedha hizo na kusababisha miradi mingi kutekelezwa chini ya
viwango na kukwamisha lengo mahususi kwa maendeleo ya jamii
Kaimaima alisema kuwa changamoto za kata ya chiwanda
anazitambua kiundani zaidi na kwamba atatumia kila njia kwa kushirikiana na
wananchi na wadau muhimu wa maendeleo kuweza kuzitatua changamoto hizo ndani ya
kata hiyo
Mwanasiasa huyo ambaye ameshawishika kushiriki kikamilifu
kuomba ridhaa ya chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) na wananchini ili waweze kumuamini na kumchagua kuwa Diwani
wa kata hiyo Mathayo Patrick Kaimaima ni mzaliwa wa kata hiyo ambaye
anazifahamu changamoto zilizopo Chiwanda ambazo zimekuwa kikwazo kikubwa kwa
maendeleo ya wananchi wa kata hiyo
Alizaliwa februari 5,1968 kijijini kwake Kwambe kata ya
Chiwanda Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma ambapo alibahatika kupata elimu ya
msingi katika shule ya Kwambe 1977-1983, baada ya hapo alipata elimu katika
chuo cha ufundi Songea (NVTC) mwaka 1986-1987 na alifanikiwa kupata cheti cha
awali cha ufundi magari( MV MACHENICAL)
Pia aliendelea na masomo yake na kufanikiwa kutunikiwa cheti
cha ufundi magari daraja la III na baada
ya hapo aliajiriwa na shirika la reli nchini (TRC) katika karakana kuu ya reli
Morogoro na alijiendeleza elimu yake ya sekondari katika kituo cha Taasisi ya
Elimu ya Watu wazima cha Morogoro na kufanikiwa kupata cheti cha Sekondari na
kuendelea na masomo ya ubaharia katika chuo cha mabaharia Dar es Salaam (DMI)
ngazi ya cheti (Marine Engineering Certificate
Baada ya kuhitimu masomo hayo alihamishiwa Mwanza na Kyera kikazi katika shirika hilo la Reli nchini
idara ya meli akiwa na cheo cha fundi mitambo wa shirika hilo, akiwa huko
alibahatika kujiendeleza na masomo ya uandishi wa habari na kuhitimu ngazi ya
cheti cha awali katika chuo cha Mbeya na kwa sasa anajishughulisha na masuala
ya ujasiliamali Mkoani Ruvuma
Hivyo kutokana na uzoefu nilionao na kufahamu changamoto za
wananchi wa kata ya Chiwanda naomba nijitokeze mbele ya chama na wananchi
kuwaomba waweze kunipa ridhaa ya kuwaongoza katika kuzitatua changamoto husika
ambazo zinaizunguka kata hiyo
Mwandishi wa Makala haya
Anapatikana kwenye simu 0755-335051
www.mangokwetu.blogspot.com
Chapisha Maoni