MTANGAZA NIA YA UDIWANI KATA YA CHIWANDA MATHAYO KAIMAIMA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUCHUKUA FOMU YA UDIWANI |
MTANGAZA NIA YA UDIWANI KATA YA CHIWANDA MATHAYO KAIMAIMA
MTANGAZA NIA YA UDIWANI KATA YA CHIWANDA MATHAYO KAIMAIMA
MTANGAZA NIA YA UDIWANI KATA YA CHIWANDA MATHAYO KAIMAIMA
NA STEPHANO MANGO, SONGEA
KADA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Wilaya ya
Nyasa Mkoani Ruvuma Mathayo Patrick Kaimaima ametangaza nia na kuchukua fomu ya
kugombea Udiwani katika kata ya Chiwanda Wilayani Nyasa ambayo kwa sasa
inaongozwa na Diwani wa Chama cha Mapinduzi(CCM) ambaye ni Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana kwenye Ofisi ya
Chadema Wilaya ya Nyasa Kaimaima alisema kuwa amechukua uamuzi huo baada ya kushuhudia
kata hiyo ikiwa na changamoto nyingi za kimaendeleo ambaye Diwani wake akiwa
ndiye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo na ameshindwa kuzitatua kwa
kipindi cha miaka 15 ya udiwani wake
Kaimaima alisema kuwa kata hiyo ni muhimu sana kwa uchumi wa
Wilaya ya Nyasa lakini miundombinu yake ya barabara kutoka makao makuu ya
Wilaya ya Nyasa ambayo ni Mbambabay
kwenda mpakani Msumbiji haipitiki na kuwafanya wafanyabiashara na wananchi kuwa
kisiwani
Alisema kuwa barabara hiyo imekuwa ni tatizo kubwa sana kwa
wananchi na hasa wakina mama wamekuwa wakijifungulia njiani na wagonjwa mara nyingi wamekuwa wakifariki
njiani kabla ya kufikishwa kwenye Hospital ya Wilaya au ya Rufaa
Alisema kuwa kumekuwa na uharibifu mkubwa sana wa mazingira
na misitu chini ya uongozi wake hivyo muda umefika wa kumpumzisha kupitia
sanduku la kura ifikapo Octoba 25 mwaka huu ili kuwakomboa wananchi wa kata
hiyo
Alieleza zaidi kuwa Diwani huyo Oddo chini ya uongozi wake
ameshindwa kuwaunganisha wananchi wa kata hiyo waliopo nje ya wilaya ya Nyasa
na ndani ya Wilaya ili waweze kupunguza kero mbalimbali za kata hiyo na badala
yake amekuwa akiwagawa wananchi hao kwa manufaa yake ya kisiasa
Alisema wakati umefika wa kuipumzisha CCM na kuipa ushindi
Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuweza kuwafanya wananchi waone
fahari kuzitumia Raslimali zao pia
waweze kufaidi umoja wa kitaifa na amani tuliyonayo watanzania
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo(CHADEMA) Wilaya ya Nyasa Jacob Beniwes alisema kuwa Chama kimejipanga
kusimamisha Wagombea wa Udiwani kwenye Kata zote 21 za Wilaya hiyo na
kumsimamisha mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Nyasa
Beniwes alisema chama kitahakikisha kinafanya kampeni usiku
na mchana ili kupata ushindi ambao utawezesha kuundwa halmashauri upya na
kuweka mifumo stahiki ya kuwaletea wananchi wa jimbo la Nyasa maendeleo stahiki
kupitia Chadema
MWISHO
Chapisha Maoni