NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WAKULIMA nchini wametakiwa kutumia pembejeo za kilimo kwa
wakati na kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo ili kukuza uzalishaji wa mazao
na kujiongezea kipato kutokana na mavuno mengi watakayoyapata
Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Kampuni
inayojishukurisha na uratibu wa kilimo Mkoani Ruvuma na uuzaji wa mbolea, mbegu
na dawa za kilimo na mifugo ya Enew Zone
Enterprises Oward Sanga kwenye siku ya mkulima iliyofanyika katika Kata ya
Sanangura Songea na kuhudhuriwa na wawakilishi wa wakulima zaidi ya 200
Sanga alisema kuwa ili wakulima waweze kuongeza uzalishaji
ni lazima watumie mbolea zao vizuri au
dawa kwa wakati kwani kilimo ndio uti wa mgongo na sekta hiyo ndio kutokana
na kuchangia katika kuondoa umaskini miongoni mwa wakulima
na kuongeza pato la Taifa.
Alisema
kuwa ukilima kwa wakati, kupanda ,kupalilia na kuweka mbolea au dawa kwa wakati
kunasababisha uzalishaji mkubwa wa mazao yote ambayo utakuwa umeyalima na
kukufanya uvune kwa wingi na kujikomboa kiuchumi
“Ili tufanikiwe katika kutekeleza malengo haya ya
kilimo, itabidi viongozi na wakulima tushirikiane kuhimiza utekelezaji wa malengo
haya na kutatua matatizo yoyote yatakayotokea mara yatakapojitokeza na hasa
katika msimu huu wa maandalizi ya kilimo,Huu ni wajibu wetu sote na hatupaswi kuwaachia
watu fulani fulani tu” alisema Sanga
Kwa upande wake Meneja Mauzo na
Masoko wa Kampuni ya mbegu ya Seed Co Kanda ya Kusini Michael Rikanga alisema
kuwa wamejidhatiti kusambaza mbegu bora kwa wakulima ili waweze kulima eneo
dogo na kuzalisha mazao mengi
Rikanga alisema kuwa mbegu hizo
zimefanyiwa utafiti wa kutosha kulingana na hali ya hewa, udongo wa maeneo
mbalimbali ya mkoa wa Ruvuma hivyo ili kufikia ustawi stahiki katika uzalisha
wa mazao ya chakula na mafuta ni muhimu wakulima wakazingatia kanuni bora za
kilimo
Baadhi ya wakulima ambao walitoa
ushuhuda kwenye siku hiyo walisema wanatambua umuhimu wa makampuni ya mbegu na
mbolea mkoa wa Ruvuma kwa namna wanavyoisaidia serikali kuwaelimisha na
kuwafanya waongeze uzalishaji wa mazao yao na kujipatia kipato
MWISHO
Chapisha Maoni