JESHI
la Polisi Mkoani Ruvuma linawashikilia watu wawili akiwemo mwenyekiti wa kijiji
wa kitongoji cha Kihongo kilichopo katika kijiji cha mapera bonde la hagati
wilayani Mbinga mkoani Ruvuma Jacobo Komba (46) kwa tuhuma za kuficha taarifa
za tukio ambalo limesababisha kifo ambacho mpaka sasa kina utata.
Watuhumiwa
waliokamata ambao wanaendelea kuhojiwa na polisi kuhusiana na tukio hilo ni
Jacobo Komba (46) ambaye ni mwenyekiti
wa kitongoji hicho na Salvanusi Mapunda ambaye ni Katibu wa kitongoji hicho.
Akizungumza
na Nipashe jana mchana ofisini kwake kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo
Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa kumi alfajiri
huko katika kijiji cha kihongo.
Alifafanua
zaidi kuwa inadaiwa katika tukio hilo Kasiani Nombo (29) aliuwawa na wananchi
ambao mpaka sasa hawajahamika ambao walijichukulia sheria mkononi kwa
kumshambulia kwa kutumia siraha za jadi wakimtuhumu kuwa ni mwizi wa kilo tano
za kahawa ambazo zilikutwa kandokando ya maiti yake zikiwa ndani ya mfuko wa
salufeti.
Alieleza
zaidi kuwa mpaka sasa inadaiwa kuwa kahawa hiyo iliyokutwa kandokando ya maiti
ya Nombo kuwa ni mali ya nani aliyeibiwa na kwamba kufuatia tukio hilo polisi
inaendelea kufanya upelelezi wa kina.
Alisema
hata hivyo kufuatia uchunguzi wa awali wa
polisi mpaka sasa haujapata ushahidi wa kuthibitisha tukio hilo ambalo
limeonekana kuwa na utata na kulazimika kuwashikilia viongozi wawili wa
serikali ya kijiji kwa tuhuma za kuficha taarifa halisi za tukio ambao bado
linaonekana kuwa na utata na kwamba polisi inaendelea kufanya upelelezi wa kina
ili kubaini kama kweli Nombo aliiba
kahawa au kuna chanzo kingine cha tukio hilo ambacho kimesababisha
mauaji hayo.
MWISHO
Chapisha Maoni