0
          KIPENZI CHA WATANZANIA EDWARD LOWASSA

SASA ni wazi kabisa Edward Lowassa hayumo tena kwenye mbio za urais ndani ya CCM baada ya jina lake kukatwa ndani ya kamati kuu kwa Zengwe kubwa na zito kutoka kwa mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete.Wagombea watano waliopitishwa ni Membe, Makamba, Magufuli, Migiro na Amina Salum.

Sote tunaamini hiyo ni njia ya kuhakikisha Membe anakuwa mshindi.Ni wazi kabisa kwa sasa Lowassa huna cha kuficha wala kupoteza, kama ni vita ya kwenda Ikulu sasa kwako ndio imeanza au imekufa.

Jaribio lako la kwanza ni kwenda kwenye Halmashauri kuu na kupinga maamuzi hayo, unayo hoja na pia unao wajumbe wa kutosha ndani ya Halmashauri Kuu, uzoefu unaonyesha kuwa ni maajabu pekee ndio yanayoweza kukurudisha tena kwenye kinyang'anyiro hicho ndani ya CCM.

Kwa sasa wafuasi wa Lowassa hawataki tena kusikia kulalamika kuwa unaonewa wala porojo za kudai hamkukutana barabarani, kwa kuwa tayari Ugali umemwagwa na Mwenyekiti kupitia kamati kuu na wewe jipange kumwaga Mboga Halmashauri kuu na ikibidi vunja kabisa na Chungu.

Chapisha Maoni

 
Top