NA STEPHANO MANGO, SONGEA
‘’Nasikitika Dunia imebeharibika na
binadamu hawana upendo wamegeuka kuwa na tabia kama za wanyama kutokana
na kukosa chembe ya upendo ambapo vitendo vya ukatili vinazidi
kukithirikiri kila kukicha mbele ya jamii.,, hiyo ni kauli yake Rehema Gwaya
(41)mkazi wa maeneo ya mtaa wa mjini kandokando ya barabara ya Sokoine Manispaa
ya Songea mkoani Ruvuma.
Rehema ambaye ni mjasiliamali mdogo
anayejishughulisha na kuuza juisi alipatwa na mkasa wa kumwagiwa mafuta ya
kupikia ya moto ambayo yalikuwa yanatumika kwaajiri ya kuchomea maandazi na mke
wa mdogo wake na mume wake baada ya kutokea sintofahamu ya usafi wa mazingira
ya nyumbani kwao kama anavyojieleza yeye mwenyewe.
Anasema tukio hilo limetokea siku ya
jumamosi Mei 30 mwaka huu majira ya saa 9 alasiri ambapo Daima Said (13)
mwanafunzi wa shule ya msingi Luseti ambaye anayeishi nae aligombana na mke wa
mdogo wake na mume wake Zafania Chimgege chanzo kikiwa ni swla la usafi wa
mazingira ambapo alipaswa kwenda kusafisha choo jambo ambalo lilisababisha
kuwepo na mzozo mkubwa hadi kufikia hatua ya kupigana na motto huyo.
Anasema kuwa wakati anarudi kutoka
kwenye biashara yake ya kutembeza juisi kwa wateja wake akasimuliwa tukio zima
lililotokea hapo nyumbani kwao wakati yeye akiwa hayupo na vijana
wanaoishi kwenye nyumba yao ya urithi jambo ambalo lilimfanya aende
akaulize kwa Zafenia ni yepi yaliyojiri ili aweze kuchukuwa hatua za kumkanya
kijana wake.
Rehema anafafanuwa zaidi kuwa kabla
ya kupata maelezo ghafla alijikuta akishambuliwa kwa maneno makali
yaliyoambatana na matusi na zefania ambaye kwa wakati huo alikuwa anachoma
maandazi kwaajiri ya biashara yake wakati anaendela kutafakari kauli chafu
ambazoalikuwa anazitoa zefania alishtuka akimwagiwa mafuta ya kuchomea maandazi
usoni na papo hapo alianguka chini na kupoteza mwelekeo jambo ambalo lilimpa
nafasi Zefania kumkali juu huku akimchubua ngozi ambayo ilikuwa imeungua kwa
mafuta na kumsababishi maumivu makali ambayo yalipoteza fahamau na
kujikuta yupo hospitali ya Mkoa Songea(HOMSO) akiwa amelazwa wodi ya wanawake
majeruhi ambako anaendelea kupatiwa matibabu.
,,Nawaomba watanzania wenye mapenzi
mema kunisaidia kwani kwa sasa siwezi kufanya shughuli ya aina yeyote kutokana
na kuuguza majeraha ya motoambayo yanamaumivu makali na hapa nilipo nina
mtoto mdogo wa miezi 9 amabaye ananyonya na pia naviomba vyombo vya dola
viangalie uwezekano wa kuona umuhimu wa kuchukuwa hatua dhidi ya mtuhumiwa
kwani nimesikia alikamatwa na kuachiwa wakati hali yangu bado ni mbaya
.’’alisema Rehema.
Anasema kuwa kwa sasa hivi biashara
yake ya ujasilia mali imesimama na hana uwezo wa haina yeyote kwani mume wake
Salum Mbaya analazimika kumuuguza muda wote kutokana na mtoto kuwa na umri wake
kuwa mdogo na muda mwingine kulazimika kumbeba wakati anapohitaji kupumzika
hivyo anaiomba serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo chama cha
waandishi wa habari wanawake nchini (TAMWA)kuona namna ya kumsaidia ili
aweze ili familia yake iweze kuboreka.
Rehema akizungumza kwa taabu
kutokana na maumivu makali aliyonayo ya majeraha ya mafuta ya moto alisema kuwa
anashukuru uongozi wa hospitali ya serikali ya Mkoa pamoja na madaktari na
wauguzi kwa kumsaidia matibabu toka amefika hadi sasa na hajaona kasoro yoyote
hivyo amewataka waendelee na moyo huo wa upendo kwa wagonjwa wote.
Naye Mume wa Rehema Salum Mbaya
anasema kuwa siku ya tukio yeye hakkuwepo nyumbani alikuwa safarini kwenye
shughuli za biashara zake ndogondogo ambako alipigiwa simu na Kakaka yake
Rajabu Mbaya kuwa nyumbani kwao kumetokea tatizo ambapo alinieleza kuwa shemeji
yangu amemmwagia mafuta ya kupikia mke wangu usoni na ameungua vibaya ikanipasa
nipande gari na kurudi nyumbani lakini nilipofika nyumbani nikakuta tayari mke
wangu wameshamfikisha hospitali ya Mkoa ambako anaendelea kupata matibabu.
“Nasikitika sana kwa tukio
lililotokea kwani limetokea nikiwa sipo nipo safari ya mbali kidogo hivyo
natumia fursa hii kuiomba jamii kwa wakati huu mgumu wa kumuuguza mke wangu
wanisaidiea lakini pia vyombo vya dora vichukuwe mkondo wake ili kukomesha
tabia hizi zinazoonekana kushika kasi katika kipindi hiki na iwe fundisho wa
watu wengine wenye tabia za vitendo vya ukatili dhidi ya wenzao kwani tukio
hili sawa na lamauawaji.”alisema Salum.
Rajabu Mbaya ambaye ni kaka wa Salum
Mbaya anasema kuwa yeye alipata taarifa toka kwa watoto kuwa huko juu kwenye
ghorofa ya kwanza watu wanapigana na wanataka kuuwana na wakati nachukwa
maamuzi ya kupandisha huko juu nikaambiwa tayari wameumizana na nilipofika
nikakuta hali mbaya jambo ambalo lilimfanya amuonye mke wa mdogo wake Afidhi
Mbaya kuwa hatua aliyoichukuwa ya kumwagia mafuta ya kupikia ya moto sio kizuri
hivyo wao kama wanafamilia hawajaridhika na tukio hilo.
Said Gwaya mkazi wa Tunduru mjini
ambaye ni kaka wa Rehema Gwaya aliyemwagiwa na mafuta ya kupikia ya moto
usoni anasema kuwa ametoka Tunduru na amekuta hali ya dada yake sio nzuri cha
kushangaza alimkuta mtuhumiwa Zafania ameachiwa na jeshi la Polisi kitendo
ambacho ambao mtuhumiwa huyo akamatwe mara moja kwani hali ya mgonjwa bado sio
nzuri.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa
hospitali ya Serikali ya Mkoa Songea Dkt. Benedkto Ngaiza amethibitisha
kumpokea mgonjwa ambaye amefikishwa hospitalini hapo akiwa na majeraha
yaliyosababishwa kumwagiwa mafuta ya kupikia ya moto usoni na kwamba kwa sasa
hivi anaendelea kupatiwa matibabu .
“Mgonjwa tumempokea kama mnavyomuona
na ameungua zaidi sehemu za usoni na anaendelea vizuri nitoe wito kwa jamii
tupendane kwani hivi vitu vya mafuta ,maji tupo navyo kila siku majumbani mwetu
tusitumia kama silaha ya kuwaumiza wengine badala yake vitumike kama
vinavyokusudiwa na si vinginevyo.”alisema Dkt. Ngaiza.
Hata hivyo alikiri kuwepo kwa
matukio ya vitendo vya ukatili na kwamba kwa tukio hili kwa mwaka huu halizi
kuwa la kumi licha ya kuwepo kwa matukio madogo madogo ya vitendo vya ukatili
hivyo ameiomba jamiii kubadilika.
Hata hivyo kamanda wa polisi wa Mkoa
wa Ruvuma Mihayo Mikhela amekiri kutokea kwa tukio hilo na mtuhumiwa tayari
anashikiliwa na polisi wakati upelelezi wa kuhusiana na tuki hilo ukiwa
unaendela na ukikamilka mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka
linalomkabili.
Aidha vitendo vya ukatili vimekuwa
vikiongezeka siku hadi siku licha ya wanaharakati kutoka Ruvuma Orphans Association(ROA)
na TAMWA kupinga vitendo hivyo lakini bado jamii inaendela kuwa na
tabia ya kufanya vitendo vya ukatili jambo ambalo tunapaswa kujiuliza je elimu
juu ya vietendo vya ukatili inawafikiwa watanzania na kama inawafikia kwa nini
vitendo hivyo vya ukatili vimekuwa vikiendela maeneo mbalimbali hapa nchini.
MWISHO.
Chapisha Maoni