Na Stephano Mango Namtumbo
Jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma linawasaka watu
watatu wasiofahamika wanaodaiwa kuwa ni majambazi ambao walivamia nyumba na
kumpiga nondo kichwani Winfrid Asilia Sanga (73) mkazi wa kijiji cha msindo akiwa
amelala na kumsababishia kifo kisha kupora fedha shilingi elfu 80,000 /=za
kitanzania .
Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo
zimethibitishwa na kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi
zilisema kuwa tukio hilo lilitokea septemba 7 mwaka huu majira ya saa 6:30
usiku huko katika kijiji cha msindo.
Alisema kuwa inadaiwa siku hiyo Sanga akiwa amelala
nyumbani kwake alivamiwa na watu watatu wasiofahamika na walimpiga nondo
kichwani kisha kopora fedha shilingi elfu 80000 ambazo alikuwa amezihifadhi
chini ya godoro.
Alisema kuwa wakati anapigwa na majambazi hao sanga
alipiga kelele ambazo zilisababisha majirani washtuke na walipofika kwenye eneo
la tukio ghafla majambazi hao walitokomea kusiko julikana.
Alieleza zaidi kuwa inadaiwa majirani ndio
waliomchukua sanga na kumpeleka kwenye Zahanati ya msindo ambako mganga wa
zahanati hiyo aliwaambia kuwa sanga alikuwa tayari ameshafariki dunia.
Hata hivyo kaimu kamanda wa polisi malimi alisema kuwa
juhudi za kuwasaka watuhumiwa zinaendelea na amewaomba raia wema waonyeshe
ushirikiano kwa jeshi la polisi ili watuhumiwa hao waweze kukamatwa.
MWISHO
Chapisha Maoni