Askari Polisi wakiteketeza bangi
Wa kwanza toka kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela, wa pili Afisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Ruvuma Revocutus Malimi,na watatu ni Afande Tossi ambaye ni \dereva wa RPC
Mtuhumiwa wa kilimo cha bangi Kilian Fussi akiwa amefungwa pingu huku akiangalia polisi wanavyofyeka bangi yake
NA
STEPHANOMANGO,SONGEA
SHAMBA
la dawa ya kulevya aina ya bangi lililopo Sanangula halmashauri ya Manispaa ya
Songea mkoani Ruvuma limefyekwa na kuteketezwa kwa moto na Jeshi la Polisi
mkoani Ruvuma huku mmiliki wake Kilian Fussi akiangalia kwa uchungu uteketwezaji
huo
Tukio
hilo la kuteketeza zao hilo haramu ambalo limekuwa likipigwa vita na viongozi
mbalimbali nchini kutokana na madhara yake yanayojitokeza kwa watumiaji na
jamii inayowazunguka lilitokea wiki iliyopita na kusimamiwa na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela na Afisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
Mkoani Ruvuma Revacus Malimi
Gazeti
hili lilikuwepo eneo la tukio wakati timu ya Polisi Mkoa wa Ruvuma ikiteketeza
zao hilo haramu ambalo limekuwa tishio kwa vijana wengi na kushuhudia mmiliki
wa shamba hilo akihuzunika wakati zoezi la uchomaji wa moto likiendelea kwenye
shamba lake ambalo lipo ndani ya mji wa Songea ambao ni maarufu kwa mji wa historian
a utalii wa utamaduni kutokana na historia ya Vita vya Majimaji vilivyopigana
na wajerumani miaka ya 1905 mpaka 1907
Baadhi
ya mashuhuda wa tukio hilo kwa nyakati tofauti
walisema kuwa Kilian Fussi amekuwa ni mkulima wa siku nyingi wa mmea huo
haramu na amekuwa akilindwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wa eneo hilo
kwani ni mara nyingi raia wema walikuwa wanazitaarifu mamlaka zinazohusika ili
ziweze kuchukua hatua lakini juhudi zao zimekuwa zikigonga mwamba
Walisema
kuwa tukio hilo limetokea inawezekana baadhi ya watu ambao anafanya nao
biashara hiyo haramu wamekorofishana na ndio maana wameamua kuitaarifu Polisi
ili waweze kumkomoa kutokana na ukulima wake wa bangi
Walisema
kuwa mara nyingi wakitoa taarifa kwa siri kwenye vyombo vya dola taarifa zao
zimekuwa zikivuja na kusababisha uhasama baani ya Fussi na baadhi ya watu ambao
wamekuwa wakitoa taarifa za kufichua ukulima huo wa bangi katika mtaa wao
Walisema
kuwa majirani wenzake ambao wanalima katika eneo moja mazao ya chakula na
biashara katika eneo hilo walijaribu kumuonya kuhusu ulimaji wa zao hilo
haramu, mara kadhaa amekuwa haonyeki na amekuwa akiishi kwa chuki na
wanaomkataza kulima bangi hiyo
Kama
kawaida yake gazeti hili lilimnasa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo
Msikhela ili aweze kuzungumzia sakata hilo la ukomeshaji wa kilimo haramu cha
bangi nchini ambacho kimekuwa kikileta madhara makubwa kwa jamii
Msikhela alikili
kutokea kwa tukio hilo mwishoni mwa wiki ambapo alisema kuwa zoezi hilo lilifanikiwa baada ya Jeshi hilo
kupokea taarifa za kuwepo kwa mashamba ya bangi katika eneo hilo na kwamba
mmiliki wa shamba hilo amekamatwa na taratibu za kisheria zinaendelea ili
afikishwe mahakamani kujibu tuhuma zake,
Kufuatia hali hiyo, Kamanda Msikhela alitoa
wito kwa watu wengine wenye mapenzi mema na nguvu kazi ya vijana wao, ambao
wamekuwa wakiathiriwa na mihadarati hiyo, kutoa taarifa za siri kwa jeshi hilo
ili waweze kukamatwa na sheria kufuata mkondo wake.
MWISHO
Chapisha Maoni