0


Na Gideon Mwakanosya- Songea

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu wawili wakazi wa kijiji cha Songambele wilayani Namtumbo kwa tuhuma za kukutwa na siraha moja aina ya Rifle 458MM ambayo namba zake zimefutika.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hasani Ally Puka(30) na Hassani Kassim Mwambungu (31) wote wakazi wa kijiji cha Songambele wilayani Namtumbo.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa za jioni huko katika kijiji cha Songambele ambako Askari wa Idara ya Upelelezi wa wilaya ya Namtumbo kwa kushirikiana na Askari wa kikosi cha kuzuia Ujangiri kanda ya kusuni wakiwa katika shughuli zao za kikazi walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na siraha moja aina ya Rifle 458MM ambayo namba zake hazisomeki kutokana na kuwa na kutu nyingi siraha hiyo ambayo pia haikuwa na risasi.

Alifafanua zaidi kuwa Bunduki hiyo iliyokamtwa ilikuwa imehifadhiwa ndani ya nyumba ya watuhumiwa kwa kuchimbiwa chini na ilikuwa inatumika katika shughuli za uwindaji haramu kwenye mbuga ya wanyama ya hifadhi ya Taifa ya Selou.

Alieleza zaid kuwa watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara tu upelelezi utakapokamilika.

MWISHO 

Chapisha Maoni

 
Top