RPC RUVUMA MIHAYO MSKHELA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
JESHI
la Polisi mkoani Ruvuma limemtia mbaroni Rajabu Mbunda(30) mkazi wa
kijiji cha Mkumbi wilaya ya Mbinga kwa tuhuma za kukutwa akiwa ndani ya
banda la Mbuzi huku akifanya mapenzi na Mbuzi jike.
Akizungumza
na gazeti hili jana mchana Ofisini kwake kaimu kamanda wa polisi wa mkoa
wa Ruvuma Revocatus Malimi alisema kuwa tukio hilo limetokea januari 18
mwaka huu majira ya saa sita na nusu usiku huko katika kijiji cha
Mkumbi kilichopo kata ya Mhukulu wilayani Songea.
Kamanda Malimi
alisema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Mbunda alikutwa akiwa ndani ya
banda la mbuzi linalomilikiwa na Twaini Mbele(45) mkazi wa kijiji
hicho.
Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo hiyo kabla ya
tukio mtuhumiwa mbunda alikuwa amekwenda kwenye nyumba hiyo kwa ajili ya
kunywa pombe kwa kuwa kwenye nyumba hiyo kuna klabu cha pombe za
kienyeji ambapo alipomaliza kunywa aliaga kuwa anaondoka na kuacha watu
wengine wakiendelea kunywa pombe akiwemo na mmiliki wa nyumba hiyo
ambaye alikuwa anaendelea kuwauzia kinywaji.
Alifafanua zaidi
kuwa inadaiwa mtuhumiwa Mbunda baada ya kuondoka kwenye kilabu hicho
alielekea kwenye banda la mbuzi ambako baadaye alikutwa na mpita njia
akifanya mapenzi na mbuzi huyo
Alieleza zaidi kuwa mpta njia huyo
ambaye jina lake limehifadhiwa wakati akipita kwenye eneo hilo la tukio
alisikia mbuzi wakipiga kelele na alipowamulika kwa kutumia tochi
alimuona mbunda akiwa ndani ya banda hilo huku akiwa amemshika mbuzi na
akiendelea kufanya mapenzi, shuhuda huyo alikimbia hadi kwenye klabu na
kuwaarifu watu waliokuwepo kwenye eneo hilo na baadaye walilazimika
kuongozana naye kwenda na kumkuta mbunda akiendelea kufanya mapenzi na
huyo mbuzi.
Alisema kuwa baadaye watu waliokuwa kwenye eneo hilo
la tukio akiwepo na mmiliki wa mbuzi huyo walifanikiwa kutoa taarifa kwa
uongozi wa kijiji hicho, ambapo walifanikiwa kumkamata na kumfungia
katika ofisi ya Kijiji na baadaye walimpeleka kituo cha Polisi kwenye
kijiji cha Magagula ambao walikamchukua maelezo ya awali na kumweka
mahabusu.
Alisema uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa
mtuhumiwa Mbunda ni mkazi wa kijiji cha Mkumbi wilayani Mbinga ambaye
inadaiwa alikuwa amekwenda kwenye kijiji hicho oktoba mwaka jana kwa
lengo la kutafuta vibarua vya kulima na kwamba muda wowote kuanzia sasa
mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa tukio hilo
kukamilika.
MWISHO
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni