NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MBUNGE wa jimbo la Songea mjini Leonidas Gama amewataka wanafunzi wa shule za msingi ,sekondari pamoja na wavyuoni wanasoma katika jimbo hilo kujenga utamaduni wa kutembelea sehemu ya makumbusho ya mashujaa wa vita vya majimaji ili kupanua uelewa wa kuitambua historia ya nchi na makabila
yake.
Wito huo aliutoa jana wakati alipoenda kuzuru makaburi ya mashujaa hao huku akiwa ameongozwa na wazee wa mila wa kabila ya kingoni ambao walimpitisha kwenye makaburi hayo kisha kumtambulisha rasimi kwenye mila na desturi kuwa ndiye mbunge wa jimbo hilo.
Gama akiwa kwenye makumbusho hayo na kuangalia kaburi lililozikiwa mashujaa 66 kwa pamoja kutokana na kunyongwa na Wajerumani February 27 mwaka 1906 wakati wa vita hiyo alisema kuwa ni vema wanafunzi
wakatumia nafasi ya makumbosho hayo kwa kujifunza kwa vitendo kwa kupata historia yenye ukweli ili kupanua uwezo wa uelewa.
Alisema inashangaza kuona wanafunzi ambao wapo karibu na makumbusho hayo kushindwa kuyatumia kikamilifu kwa kujifunzia na badala yake baadhi ya wanafunzi ambao wa maeneo yasiyo na makumbusho hayo wamekuwa wakifunga safari kwenda kutembelea makumbusho hayo.
“Mimi kama mbunge nawaambieni wanafunzi wanaosoma jimbo hili kuwa wajenge tabia ya kwenda kuangalia makumbusho hayo kwa kujifunza historia ambayo itawapanua kutambua namna ya kufanikiwa kuweka utalii“alisema Mbungea Gama.
Kwa upande wake moja ya wanafamilia ambaye ni kitukuu cha shujaa Mbano Songea ambaye ni Yasin Mbano akizungumza na MTANDAO HUU alisema kuwa mashujaa walionyongwa walikuwa 67 na waliozikwa kwenye kaburi moja ni 66 huku babu yao Mbano Songea alizikwa kaburi lingine baada ya kuuwawa siku ya tatu .
Yasin alifafanua kuwa baada ya babu yao Mbano Songea kuzikwa kwenye kaburi lake ilipofika siku ya saba Wajerumani walilifukua kaburi hilo kisha walikata kichwa na kuondoka nacho kwenda nacho Ujerumani na hadi sasa hakijaurudi na familia inaendelea kufuatilia.
Familia pamoja na ndugu na jamaa wa kabila la kingoni wanaendelea kufuatilia ili fuvu la kichwa hicho
lirudishwe ili lihifadhiwe kwenye eneo la makumbusho ya vita vya majimaji
MWISHO
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni